BANDA MEDIA BLOG

SIMBA YAIOMBA NDEGE SERIKALI, YADAI YANGA INAPENDELEWA


Akizungumza nje ya Bunge 🗣️

Naibu waziri wa wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema baada klabu ya Yanga kuomba sapoti ya kusafirisha mashabiki wao kwenda South Africa,  klabu ya Simba SC pia imeiomba Serikali iwape ndege itakayowapeleka mashabiki na timu Nchini Egypt 🇪🇬

Mwinjuma amesema, lilikuwa ni suala la utaratibu, Yanga wao waliomba mapema lakini Simba walikuwa kimya.. Ombi hilo la Simba SC watalifanyia kazi 

Pia, katibu mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo,  Gerson Msigwa akiongea na Clouds fm radio Aprili 2,2024 amesema ..

"Tumeona mitandaoni mashabiki wa Simba 

Sc wakiwa wamechukizwa kwa Serikali kuwasafirisha mashabiki wa Yanga SC, wakidai wao wametengwa na Serikali, wasifanye hivyo. Serikali ni ya wote"

"Yanga wao walituma maombi mapema tukalishughulikia suala hilo kwani tunataka timu zetu zifanye vizuri .. Simba wao hawakuleta maombi, tumepokea barua yao tutaangalia namna ya kuwachangia ili nao wawasafirishe mashabiki"Imesema Taarifa ya Gerson Msigwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG