|
|
A JOHN BANDA, DODOMA
.................................................................................
NA JOHN BANDA, DODOMA
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la
kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax Leo Aprili 3, 2024 Ametangaza Mafanikio ya
Wizara hiyo iliyoyapta ndani ya miaka 60 ya Muungano Tanzania.
Akitangaza Mafanikio ya Wizara
hiyo ambayo ilianzishwa mara baada ya Taifa kupata Uhuru mwaka 1961 huku Waziri
wake wa kwanza akiwa Oscar Kambona, mbele ya Waandishi wa Habari Jijini Dodoma
Dkt. Tax amesema Nchi inapoadhimisha miaka 60 ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Wizara ya Ulinzi na JKT ina kila sababu ya kujivunia Mafanikio makubwa iliyoyapata
ndani ya vipindi vyote 6 vya uongozi.
Amesema Awamu ya Kwanza
ilijenga Nchi, Umoja wa Kitaifa, iliunda Jeshi, Iliindaa Vijana kwa ajili ya
Ulinzi wa Nchi yao ambao walimshinda Nduli Iddi Amin Dadaa, mafanikio hayo
yakiendelezwa katika Awamu zilizofuata.
Amesema katika Kulinda Mipaka
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uhuru na Usalama wa Nchi, Wizara kupitia JWTZ
Imechangia katika kujenga Uchumi Imara ambapo wananchi hujishughulisha na
Shughuli za Uzalishaji Mali bila Hofu, Yote yakiwezeshwa na Sera, Sheria,
Kanuni na Mipango Madhubuti katika Ulinzi wa Nchi.
Pia Serikali Kupitia Wizara
imeendelea kutekeleza na Kuimarisha jeshi kwa Kulipatia Zana na vifaa Bora vya
Kisasa, Rasilimali watu na Nyenzo za Sheria ya Ulinzi wa Taifa (NATIONAL DEFENCE Act (NDA).
Amesema Ili kuimarisha Jeshi
Serikali Kupitia Wizara Imeendelea Kuboresha Maslahi kwa Wanajeshi na Watumishi
wa UMMA Kadri uwezo wa Kifedha unavyoruhusu, kwa kuwapatia makazi Bora kwa
kuwajengea Nyumba, Pamoja na Stahiki mbalimbali, Kuwapandisha Vyeo kulingana na
sifa, Vigezo na Taratibu zilizopo.
Aidha Dkt. Tax ameainisha
Ujenzi wa makazi bora kwa wanajeshi katika kambi mbalimbali za Jeshi zilizopo
kwenye Mikoa ya Arusha, Dae es laam, Dodoma, Kagera, Kigoma, Morogoro, Mwanza,
Pemba, Pwani, Rukwa, Tabora na Tanga ambapo Ujenzi wa nyumba hizo umepunguza kwa
kiasi kikubwa uhaba wa nyumba Pamoja na changamoto zitokanazo na Wanajeshi
kuishi Uraiani.
Ameongeza kuwa Mchango mkubwa
wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania katika miaka 60 ya Muungano, ni Ulinzi Madhubuti
wa Mipaka yetu, Uhuru na Katiba. “nchi imeendelea kuwa imara na yenye amani
katika awamu zote 6”, amesema
Ameyataja mafanikio mengine
kuwa ni Pamoja na Wizara kupitia taasisi zake hususani JWTZ, kukabiliana na
majanga au maafa kwa kutoa msaada wa uokoaji na ile ya kibinadamu kutokana na
taratibu zilizowekwa, ambapo linashirikiana na asasi za kiraia katika miradi ya
kimkakati Pamoja na utoaji wa huduma za afya kwa raia wanaoishi katika maeneo
ya jirani na kambi za jeshi.
“ takwimu zinaonyesha kuwa
Raia wanaopata huduma katika hospitali za jeshi ni asilimia 80”, amesema
Ametanabaisha kuwa Serikali
ya awamu ya 6 inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kipumbelea cha
ujenzi wa makao makuu ya Ulinzi wa Taifa ambao unatekelezwa na wataalamu wa
ndani ya Nchi kwa Garama ya Serikali “hili ni jambo muhimu ni mafanikio ya kujivunia
kwani ni isahara ya uimara wa Taifa letu”, amesema na kuongeza.