Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Prof.Provident Dimoso akielekeza jambo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya mfumo wa kufundishia wa Learning Management System Moodle leo Juni 11,2024 jijini Dodoma
...............
NA JOHN BANDA, DODOMA
CHUO cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) kimewaita
Wahadhiri wake jijini Dodoma kwa ajili ya Kuwafundisha Namna ya kufundisha
wanafunzi wake kwa njia ya Tekinolojia.
Akiongea wakati
alipokuwa akiyafungua mafunzo hayo, Makamu Mkuu wa Chuo,Taaluma, Utafiti na
Ushauri Elekezi wa Chuo cha IRDP Prof.Provident Dimoso amewataka wahadhiri hao kujifunza
na kuhakikisha wanauelewa mfumo huo wa Learning Management System Moodle utakaowarahisishia
kufundisha.
Katika mafunzo hayo watakayofundshwa kwa wiki moja
yakiwajumuisha Wakuu wa Idara, Maofisa TEHAMA na wale wa maktaba, Profesa. Dimoso amesema yatakuwa na tija kubwa
kwa walimu kwenye ufundishaji lakini pia kwa wanafunzi wenyewe
"Niwaombe mjifunze haya mafunzo vizuri kwa
kuuliza maswali mengi na mhakikishe mnaifahamu hii Teknologia ambayo kwa Chuo
cha Mipango tunaanza na Moodle,lakini naufahamu zipo Learning System
nyingi"amesema.
Aidha Prof.Dimoso ameeleza kuwa Chuo hicho kinaelekea kwenye kutumia Learning Management System ninyi ambao mmepata nafasi ya kujifunza tunatarajia mtauelewa huu mfumo na kwenda kuwafundisha wahadhiri wengine.
Ameongeza kuwa wanafunzi watakaoanza mwaka huu chuoni hapo watatumia mfumo huo
na wao wahadhiri watatumia mfumo huo kuwafundisha namna ya kutumia mfumo huo.
Katika hatua nyingine Prof.Dimoso amezitaja baadhi ya
faida za mfumo huo wa Learning Management System kuwa ni pamoja na idadi ya
wanafunzi kuongezeka ,lakini pia mapato ya Chuo yataongezeka na ubora wa
taaluma unaotolewa utaongezeka kwa kutengeneza wataalamu wengi wenye Weledi.
Awali akimkaribisha Makamu Mkuu wa Chuo hicho,
Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo na Mratibu wa Mafunzo hayo Said Panga
ameeleza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Elimu ya juu
kwa mabadiliko ya Kiuchumi (HEET),hasa katika eneo la kuwajengea uwezo
wahadhiri kwa kuwapa mafunzo ya muda mrefu na mfupi.
Aidha kwa upande wa mafunzo ya muda mrefu wahadhiri 5
wemewezeshwa kusoma shahada za uzamivu,
Vile vile mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wahadhiri katika mbinu bunifu
za ufundishaji na namna ya kutumia majukwaa ya TEHAMA katika kufundisha na
kujifunzia kwa wanafunzi na mfumo huo utawawezesha wahadhiri kufundishia hata
wakiwa nje ya eneo la Chuo.
Kwa upande wake Mkufunzi Msaidizi wa Chuo hicho Musa Sadica amesema kuwa kupitia mfumo huo atakuwa popote duniani na kuweza kufundisha bila shida na hata wanafunzi watakuwa wakipakua masomo kwenye mtandao hali itakayowasaidia kusoma kwa urahisi.