Katibu mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi akiteta jambo na Mgombea Uras wa Chama cha Frelimo cha Nchini Msumbiji, Daniel Chapo ambaye amefika Nchini kwa ajili ya kukitembelea Chama hicho Kikongwe.
....................
NA JOHN BANDA, DODOMA
Daniel Chapo anagombea nafasi ya Urais wa Nchini Msumbiji baada ya jina lake kuteuliwa na chama chake cha Frelimo kutokana na Wito wa Rais Filipe Nyusi mwenye umri wa miaka 64, ambaye alitangaza kutogombea nafasi hiyo katika mhula wa Tatu.
Chapo mwenye Taaluma ya Uandishi wa Habari na Utangazaji wa Radio atashiriki katika uchaguzi huo mkuu utakaofanyika Octoba 9,2024 baada ya Kuteuliwa kugombea nafasi hiyo akiwa mkuu wa Mkoa wa Inhambane nchini Msumbiji na kwamba akichaguliwa kushika nafasi hiyo ya juu kabisa katika serikali pia atakuwa ndiye Mkuu wa Chama Chake cha Frelimo.
Mgombea huyo wa Urais aliyezaliwa Januari 1,1977 mwaka huu wa uchaguzi amefikisha umri wa miaka 44, ambaye anatajwa kuwa ni mmoja wa wagombea wenye umri mdogo kugombea nafasi hiyo ya juu kitaifa, yupo Nchini Tanzania Kukitembelea Chama cha mapinduzi (CCM) kutokana na Mahusiano makubwa yaliyojengeka kati yake na Frelimo, Tangu walipokuwa wakipigania Uhuru wa Nchi yao kwani waliweka makambi yao Kongwa mkoani Dodoma na Iringa.
Wadadisi wa mambo wanasema Mgombea huyo amelazimika kuja CCM, ili kuchukua Ubani utakaomuwezesha kushinda nafasi hiyo ambayo Chama cha Frelimo kitakuwa kikimenyana na Chama Kikuu cha Upinzani cha Renamo.
Mgeni huyo aliyepokelewa na Viongozi mbalimbali pamoja na wananchama wa CCM, baadae alipata nafasi ya kusalimia.
"karibu Marafiki zetu, CCM na Frelimo ni Marafiki wa Muda Mrefu kuanzia kwa waasisi wa nchi hizi zillipokuwa zikipigania Uhuru", amesema Dk. Nchimbi