NA JOHN BANDA, SINGIDA
KANISA la Mungu limeingiliwa na Imani Mbalimbali zikiwemo za Upotoshaji zinazoharibu Imani ya kweli, kwa baadhi ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu kuiaminisha jamii ijikite kwenye matumizi ya Chumvi, Unga, Maji, Mafuta na vinginevyo vinavyoitwa vya upako kwa Garama ya Fedha.
Askofu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Rifty Valley mkoani Singida, John Lupaa ndiye aliyelimulika hilo wakati alipokuwa akihubiri katika ibada ya Jumapili iliyoambatana na utoaji wa Misaada iliyotolewa na kanisa hilo, kwa Wahanga wa Mafuriko yaliyosababishwa na Mvua zilizoambatana na Upepo mkali katika Kijiji cha Sasajila, Kata ya Chikuyu, Wilaya ya Manyoni, Januari Mwaka huu.
Akihubiri katika kanisa la Mtakatifu Methew kijijini hapo Askofu huyo, amesema hivi sasa kuna Tatizo kubwa kwa kanisa kuingiliwa na Imani potofu za matumzi ya vifaa vya kiroho huku wahusika wakihitaji malipo ya Fedha ili kugawa upako.
Amesema wapo watu wanajiita Watumishi, Mitume, Manabii, Wachungaji na Maaskofu wanaopotosha Umma kwa Makusudi wakiwaaminisha kuwa kuna upako kwenye Chumvi, Mafuta, Maji, Unga, Vitambaa, Udongo na vinginevyo ambavyo wanaweka Nembo zao na kuwauzia watu kwa garama kubwa wakidai vina upako kitu ambacho si cha kweli.
Katibu wa Ushirika wa Kikristo (UMAKI) anaeshughulika na kuratibu maendeleo ya wanawake, watoto na jamii Lay Canon Dkt. Margareth Ndonde akiimba moja ya nyimbo zilizomo kwenye albamu yake ya Mungu wetu ni wa ajabu, katika ibada hiyo
“ndugu zangu huku vijjini inawezekana hayo hayapo sana lakini huko mijini kuna sarakasi na vitimbi vingi vya upotoshwaji wa kiimani, kwa kutumia mafuta, unga, udongo, maji na vifaa vingine vinavyoitwa vya upako tena hata kumuona nabii au mtume lazima ulipe kiasi cha fedha ndipo uruhusiwe kumuona”, amsema
Aidha Askofu Lupaa amesema Vitendo hivyo ni vya kibiashara, ambapo wamebuni namna ya kujipatia fedha kwa njia hiyo lakini si kuwasaidia watu bali kuwanyonya fedha na mali zao.
Amesema kama ilivyo kwa wazo la somo la Jumapili kuwa ni uongozi wa Nguvu za Roho mtakatifu, huku Akinukuu Maandiko kutoka kwenye kitabu cha LUKA 6:43,45 kuwa Mtawatambua kwa Matunda yao na kwamba huwezi kuchuma Zabibu kwenye Mchongoma na Tini kwenye Mti wa Miiba, ndivyo huwezi kupata kitu kutoka kwao ila kwa Mungu.
“upako wa kweli unatoka kwenye nguvu za Roho mtakatifu, msikubali kupotea bure watu hawa wanajulikana kiurahisi kutokana na matangazo yao madhabahuni, kwenye vyomba vya Habari na kwenye mitandao ya kijamii wakionyesha wazi wana uchu wa fedha zenu kwa kutaja kiasi cha fedha za kuanzia elfu 10, mpaka Malaki ya fedha ndiyo upate huo upako,
Tena wengine ili uweze kuwaona lazima utimize masharti ya kulipa fedha mlangoni”, amesema.
Katibu wa Ushirika wa Kikristo (UMAKI) anaeshughulika na kuratibu maendeleo ya wanawake, watoto na jamii Lay Canon Dkt. Margareth Ndonde akiimba moja ya nyimbo zilizomo kwenye albamu yake ya Mungu wetu ni wa ajabu, katika ibada hiyo, huku akisapotiwa na waimbaji wengine akiwemo Mke wa Askofu Devota Lupaa..