
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda akipewa maelezo ya ufanisi wa Silaha za kivita za Jeshi la Ukombozi la watu wa China katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda (kushoto) akimkabidhi Bendera ya Taifa Mkuu wa Mazoezi ya medani, Umoja 2024 Meja Jenerali Fadhili Omar Nondo wakati akifungua Mazoezi ya medani, Umoja 2024 leo Julai 29, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani kwa ajili ya kuadhimisha Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Ushirikano wa Jeshi la Ukombozi la watu wa China.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda (kushoto) akizungumza jambo leo Julai 29, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wakati akifungua Mazoezi ya medani, Umoja 2024 wanaoshiriki Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Jeshi la Ukombozi la watu wa China kwa ajili ya kuadhimisha Miaka 60 ya JWTZ pamoja na Ushirikano na Nchi ya China.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Ibrahim Michael Mhona akizungumza jambo leo Julai 29, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wakati wa ufunguzi wa Mazoezi ya medani, Umoja 2024 wanaoshiriki JWTZ pamoja na Jeshi la Ukombozi la watu wa China kwa ajili ya kuadhimisha Miaka 60 ya JWTZ pamoja na Ushirikano na Nchi ya China.

Msaidizi Mkuu wa Majeshi, Jeshi la Ukombozi la watu wa China Meja Jenerali Ye Dabin akizungumza jambo leo Julai 29, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wakati wa ufunguzi wa Mazoezi ya medani, Umoja 2024 wanaoshiriki ni JWTZ pamoja na Jeshi la Ukombozi la watu wa China kwa ajili ya kuadhimisha Miaka 60 ya JWTZ pamoja na Ushirikano na Nchi ya China.

Jeshi la Ukombozi la watu wa China wakiwa katika picha ya pamoja.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika picha ya pamoja.

Makomando wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani katika ufunguzi wa Mazoezi ya medani, Umoja 2024 na Jeshi la Ukombozi la watu wa China

Picha za matukio mbalimbali wakati wa ufunguzi wa Mazoezi ya medani, Umoja 2024 iliofanyika leo Julai 29, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani (Picha na Noel Rukanuga)
