Baada ya Kusikiliza na Kutatua Kero kwa Miezi Mitatu, Tulibaini kuna Migogoro Mingi iko katika Mhimili wa Mahakama tukabaini watu wetu wengi wanapoteza Haki zao, Stahiki zao na Kudhulumiwa Mali zao
Tumefanya Utafiti Tumepata Majibu kwamba uelewa wa Mambo ya Kisheria kwa Wananchi wetu ni wa wastani jambo linalopelekea Jamii yetu kukosa USAWA NA HAKI
Tumeamua Kuanzisha Kampeni Maalumu ya Kila ALHAMISI katika kila Juma Tutakuwa na Zoezi, Kampeni na Utaratibu wa Kusikiliza na Kutatua Kero na kwa MIGOGOGORO ILIOPO Katika Mhimili wa Mahakama Tutatoa MSAADA WA KISHERIA kwa wenye uhitaji, tumewasiliana na wenzetu wa TLS pamoja Kituo Cha Law School ili kupata wanasheria watakao saidiana na wanasheria wetu wa Manispaa ya Ubungo", amesema DC Ubungo wakati Zoezi la Utoaji wa Elimu likiendelea huko Mbezi Luguluni
Kazi Inaendelea







