........
NA JOHN BANDA, DODOMA
MWENYEKITI wa Bodi ya Benki ya Ushirika ya
Kilimanjaro (KCBL) Prof. Gervas Machimu amewaalika wanahisa wa Benki hiyo
kuhudhuria kwenye mkutano mkuu wa 27
unaotarajiwa kufanyika jijini Dodoma hapo kesho julai 26,2024
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Hapa, leo
Julai 25,2024 Mwenyekiti huyo amesema kuwa mkutano huo utakaofanyika kesho unalengo
la kuwaeleza mafanikio ya utekelezaji na utendaji wa benki hiyo ikiwa ni Pamoja
na kufahamu au kujua uelekeo wake katika mwaka unaofuta.
Amesema Benki hiyo imetanua wigo wa kujiendesha
kibiashara kwa kugusa miradi mingi ya kimkakati na Kilimo Biashara ikiwemo cha
kahawa, korosho, Pamba, na Tumbaku ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Kuwa Waziri wa
Kilimo Husein Bhashe.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Banki Hiyo Godfrey Ng’ulah amesema Benki hiyo imefanikiwa katika uendeshaji kimfumo, utawara bora na tija ambapo mkutano huo unatarajiwa kuwa na wajumbe kutoka vyama vikuu vya Vikuu vya Ushirika Union, AMCOS, vyama vya msingi vya Kilimo, Vyama vya akiba na Kukopa, wamiliki hisa KCBL, wanaushirika na wananchi wa kawada watapata fursa ya kujulishwa namna inavyofanya kazi.
Amesema BENKI YA USHIRIKA YA KILIMANJARO COPARATIVE
BANK LIMITED (KCBL) ambayo ilianzia kule Moshi Mkoani Kilimanjaro hivi sasa
inaungana mabenki mengine ya Ushirika na kuwa Benki kuu ambayo makao makuu yake
yatakuwa jijini Dodoma
Ameongeza kuwa Mkutano huo unatarajiwa kufanyika ukumbini
na kwa njia ya Mitandao ya kijamii ambayo itawapa fursa ambao hawatafika kuufuatilia
na kutoa maoni yao.
Amesema wajumbe watapata nafasi ya kusomewa Taarifa
ya utendaji kazi ya mwaka 2023, safari ya miaka mitatu ya mageuzi ambapo Benki ya KCBL Pamoja na Benki ya Tandahimba zitaungana
na kuwa Benki Kuu ya Ushirika.