BANDA MEDIA BLOG

MOJA YA VIBAO VYA ZILIZOPENDWA VYA MAREHEMU MARIJANI RAJABU NI NDOA YA MATESO ILIYOMCHOSHA NA KWENDA KUSHTAKI KWA MJUMBE JE KWA KOCHA MGUNDA???


NIMEKUWA Muumini wa Nyimbo za Kizamani mpaka naweza Kusema Nimeongeza Hekima Nyingi Kutoka kwa Watunzi wa Kale.

Maisha ya Mwalimu Juma Mgunda na Simba Naweza Kuyafananisha na Kibao cha Marijani Rajabu 🎚️NDOA YA MATESO.

Marijani Rajabu katika Kibao chake cha 🎚️NDOA YA MATESO alivaa Uhusika wa Mwanamke ili aweze Kueleza Mateso anayopitia kwa Mumewe.

🎶Niulizieni Enyi Walimwengu.Huyu Mwanamume anavyonitsa"Hii ndiyo haki au ni Mateso X2.🎶Kanitoa Kwetu kwa Baba na Mama kwa Vigelegele na Heshima Nyingi"Mtizameni sasa anavyonigeuka.

©Marijani Rajabu

Mwalimu Juma Mgunda Mbali na Takwimu safi katika Kikosi cha Simba Heshima yake Imegeuka kama Kata la Chooni.

☑️Kocha Mkuu _ Fadlu David's

☑️Kocha Msaidizi _ Darian Wilken

☑️Kocha wa Makipa _ Wayne Sandalands

☑️Kocha wa Viungo _ Riedoh Berdien 

☑️Mchambuzi _ Mueez Kajee 

Simba hilo ndiyo Benchi lao Jipya la Ufundi Makocha wote ni Raia wa Afrika Kusini Yaani Fadlu David's kaja na Benchi lake.

Takwimu za Juma Mgunda.


🤳️2-2 Vs Namungo FC

☑️2-0 Vs Mtibwa Sugar FC

☑️2-0 VS Tabora United FC

☑️3-0 Vs Azam FC.

🤳️1-1 Vs Kagera Sugar FC

☑️1-0 Vs Dodoma Jiji FC

☑️4-1 Vs Geita Gold FC

☑️1-0 Vs Kinondoni MC

☑️1-0 Vs JKT Tanzania FC

Juma Mgunda tangu akabidhiwe timu katika Mchezo wa Namungo FC Hajapoteza Mchezo wowote Katika Michezo 9.Alistahili Kitengo.

Simba Wamemuahidi Juma Mgunda Watampa Majukumu Mengine.

Juma Mgunda ni Kocha Mzuri ambaye ana Uwezo wa Kufundisha Vilabu Vingi vya Ligi Kuu ya Tanzania Bara ila ndiyo hivyo NDOA YA MATESO.

Marijani Rajabu aliichoka NDOA YA MATESO na akaenda Kumshitakia MJUMBE.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG