BANDA MEDIA BLOG

NAIBU WAZIRI AKEMEA WIZI DIRA ZA MAJI MWANZA


Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa MWAUWASA, Mhandisi Robert Lupoja (kulia),leo akimweleza Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Matthew (katikati),ufanisi wa kituo hicho.
Watumishi wa MWAUWASA wakisiliza maelekezo ya Naibu Wairi wa Maji, Mhandisi Kundo Matthew (katikati), leo alipoakagua miundombinu ya maji Manispaa ya Ilemela.
Katibu Tawala wa Ilemela, Wakili Mariam Msengi,leo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Hassan Masala, akizungumza na baadhi ya wananchi wa Lumala wakiwemo watumishi wa MWAUWASA.Kuli kwake aliyeketi ni Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Matthew.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Lumala,Manispaa ya Ilemela,Zakayo Kasiri, akitoa kero ya mgawo wa maji kwa Naibu Waziri wa Maji,Mhandisi Kundo Matthew,leo alipofanya ziara katika mtaa huo.
Naibu Waziri wa Maji,Mhandisi Kundo Matthew, akifungua koki ya maji leo, katika eneo la mlima wa Rada ili kujiridhisha kama maji yanatoka,nyuma ni Mkurugenzi wa MWAUWASA,Neli Msuya na mbele ya Naibu Wazri ni Justina Mbise,mama mwenye nyumba hiyo.
7.Pic 08-Naibu Waziri wa Maji,Mhandisi Kundo Matthew, akikwea ngazi kwenda kukagua tangi la maji la mlima wa Rada wilayani Ilemela, leo. (Picha na Baltazar Mashaka)
……
NA BALTAZAR MASHAKA,ILEMELA

NAIBU Waziri wa Maji,Mhandisi Kundo Matthew,amekerwa na vitendo vya wizi wa dira za maji na kuisababishia serikali hasara,huku akiwataka wananchi wa Wilaya ya Ilemela na Jiji la Mwanza,kujiepusha navyo.

Pia amewataka wananchi wawe walinzi wa miundombinu ya miradi ya maji na kulipa Ankara za matumizi kwa wakati,miradi iwanufaishe na kuwa endelevu.

Mhandisi Kundo ametoa kauli hiyo leo,alipozungumza na wananchi wa Kata ya Buswelu katika mkutano wa hadhara uliolenga kusikiliza na kutatua changamoto na kero za maji zinazowakabili wa wananchi wa Ilemela na Jiji la Mwanza.

Amesema serikali haitakuwa kikwazo kwa wananchi kupata maji,imedhamiria kila mwananchi apate huduma hiyo karibu lakini wizi wa dira za maji unaisababishia serikali hasara.
“Wizi wa dira za maji,ni mali ya mamlaka na zina gharama kubwa,tusaidieni kuwa walinzi wa dira hizo,kazi yetu ni kuwasogezea huduma karibu,msiharibu miundombinu ya maji hata kama una hasira usizihamishie kwenye mabomba,”amesema Mhandisi Kundo.

Amesema rasilimali ya maji ni uhai,inazalishwa kwa gharama kubwa,hivyo wananchi wasikwepe kulipa badala yake wadhibiti matumizi watumie kulingana na uwezo wa kipato.

“Msidanganyike kutoa fedha (rushwa) kuficha madeni kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu,deni lako halisi haliwezi kufutwa katika mfumo tusikwepe,tukatumie kulingana na kipato,tukifanya hivyo malalamiko ya kubambikizwa Ankara yatapungua,”amesema Naibu Waziri huyo wa Maji.

Amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa fedha za miradi ya sekta ya maji,lakini tatizo la uhaba wa maji jijini Mwanza,chanzo chake hakitoshelezi,mradi wa Igombe-Kabangaja ukikamilika utaondoa changamoto hiyo kwa kutoa maji ya uhakika.

Mhandisi Kundo ameeleza kuwa changamoto haziwezi kwisha kwa wakati mmoja,uhaba huo wa maji unasababishwa na ongezeko la idadi ya watu na makazi mapya pia,uzalishaji usiokidhi mahitaji.

“Niwashukuru kwa kuwa wakweli na serikali haitawangusha,nchi hii hatutaijenga kwa kudanganyana na ukweli utatusaidia kujenga badala ya kubomoa,uchungu na hisia zenu hatutazipuuza tutaendelea kuzifanyia kazi kwa kuongeza mtandao wa maji licha ya changamoto ya bajeti,”amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (NWAUWASA),Neli Msuya amesema mradi wa Matokeo ya Haraka unaogharimu sh.bilioni 4.7 umechelewa kukamilika sababu ya ukosefu wa fedha.

“Sh.milioni 500 zilitolewa kuboresha mfumo wa maji Buswelu,kutokana na ukubwa wa tatizo fedha hizo hazikukidhi kufikisha maji maeneo yote,tulibuni Mradi wa Matokeo ya Haraka wenye thamani ya sh.bilioni 4.7,tumepokea sh.bilioni 1.7 tukalaza mabomba kilometa 14,”amesema.

Naye Mbunge wa Ilemela (CCM),Dkt.Angeline Mabula amesema juhudi za Rais Dk.Samia kumtua mama ndoo kichwani zimeanza kuonekana ambapo Ilemela imepata mradi wa Maji wa Igombe-Kabangaja wenye thamani ya sh.milioni 800 ukikamilika pamoja na chanzo cha Butimba,maji yatatosheleza.

“Tunaishukuru serikali kwa Mradi wa Matokeo ya Haraka,umekuwa na tija kwa kupunguza kero ya maji,changamoto ni vifaa na naamini itatatuliwa,niombe Mkurugenzi wa MWAUWASA mifumo ikifunguka fedha zikaanza aje hapa Buswelu kuondoa tatizo la maji,”amesema.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG