BANDA MEDIA BLOG

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KILIMANJARO CHANADI MAZIWA YA MTINDI LISHE YANAYOPONYA HOMA ZA MATUMBO NA KUONGEZA SELI MWILINI.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wa Dodoma Rosemary Senyamule akionyeshwa Mtindi lishe (YOBA) na Mwenyekiti wa Chama cha Mamba kilicho chini ya  Dairy Cooperative Society LTD kinachojishughulisha na Ufugaji Pamoja na ukusanyaji wa maziwa na  kisha kuyasindaka, Mercy Mwanga, alipotembelea Banda la WE EFFECT Nane -nane nzuguni 

                                            ..................

NA JOHN ISRAEL, NANE- NANE DODOMA

CHAMA kikuu cha Ushirika Mkoani Kilimanjaro  Kikiwezeshwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo WE EFFECT kimeendelea kupiga kambi katika Viwanja vya Nane – nane Nzuguni jijini Dodoma kunakofanyika Maonyesho ya Wafugaji na Wakulima huku kikitamburisha Bidhaa ya Mtindi Lishe

Mtendaji Mkuu wa Chama hicho chenye Mjumuiko wa Vyama vya Msingi 17 vinavyojihusisha na Ufugaji wa Ng’ombe wa Maziwa, Erenesti Haule akiongea kwenye Maonyesho ya Nane-nane jijini Dodoma, amesema katika vyama hivyo wanasindika Bidhaa za Maziwa ambapo yanasindikwa kwa virutubisho maalumu vinavyosaidia maswala ya kiafya kwa Watoto na wazee.

“tunasindika maziwa salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu, yakitengenezwa na kimea maalumu kwa ajili ya kutibu homa za matumbo kwa Watoto na wazee”, amesema mtendaji huyo

Aidha amesema soko la maziwa hayo lipo  Mkoani Kilimanjaro,  na kwamba kama chama wameanza juhudi za kusaka masoko katika mikoa mingine kwakutumia maonyesho mbalimbali ya Biashara yakiwemo maonyesho ya Maziwa, maonyesho ya Ushirika na ya Wakulima na Wafugaji Nane-nane yanayofanyika kitaifa na kikanda ambapo kumekuwa na mwitikio mkubwa.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mamba kilicho chini ya  Dairy Cooperative Society LTD kinachojishughulisha na Ufugaji Pamoja na ukusanyaji wa maziwa na  kisha kuyasindaka, Mercy Mwanga amesema  Mtindi lishe aina ya YOBA Halisi na Yoghat wanaitengeneza kwa usahihi baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Maendeleo la EFFECT

Amesema kutokana na Kimea hicho kinachowekwa kwenye Mtindi lishe, kimesababisha faida nyingi za Kiafya zinazotokana na Bidhaa hiyo ya maziwa inayojulika kwa jina YOBA.

“mtindi lishe huu unaotengenezwa na kirutubisho maalum unatumika kama chakula, kiburudisho na tiba kwani unashibisha, pia unatibu vidonda vya tumbo, kuondoa Gesi, unaongeza seli zilizopungua na kuondoa sumu mwilini”, amesema

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG