NA JOHN BANDA, DODOMA
.......................................
WANANCHA wa chama cha Mapinduzi CCM, katika matawi ya Iyumbu na Nyerere kata ya iyumbu jijini Dodoma leo Oct 23,2024 wamepiga kura za maoni kwa ajili ya kupendekeza majina ya makada wa chama hicho yatakayopelekwa kwenye vikao vya kamati za siasa ngazi ya tawi, kata mpaka wilaya kwa ajili ya Uteuzi wa watakaogombea uongozi wa serikali za mitaa, huku wakiwabwaga waliokuwa wenyeviti wa mitaa wawili waliomaliza muda wao na kuwarudisha wengine wawili.
Mwenyekiti wa CCM, kata ya Iyumbu, Sadiki Mponyamili akiuongelea ucjhaguzi huo uliojumuisha wajumbe wa serikali za mitaa, amesema uchaguzi umeenda vizuri katika matawi yote mawili na kwamba Wanaccm Wameendelea kuwaamini na kuwapendekeza Makada wawili wa chama hicho Ayubu Mandabaga katika mtaa wa Nyerere na Venasi Mwibala mtaa wa UDOM, huku wakipendekeza sura mpya za Jairosi Mnyamili mtaa wa Mwinyi na Nasson Mwibala maarufu Lugunyale katika mtaa wa Iyumbu.
amesema Maoni ya Wajumbe yatazingatiwa katika vikao vyote kuanzia na vile vya Tawi hadi kata kabla ya kuyawasilisha Wilaya kwa ajili ya uteuzi, "kubwa niwaombe wajumbe na wanaccm kuondoa wasiwasi waendelee kuvumilia wakati wanasubiri maamuzi ya vikao vitakavyofuata", amesema
katila mapendekezo hayo aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa wa Iyumbu George Makapi pamoja na Moses Masuma wa mtaa wa Mwinyi kura walizopata hazikutosha kuwarudisha katika nafasi zao walizozitumia
Awali baada kura kupigwa katika ukumbi wa Kurongoni Baa Mwenyekiti wa Uchaguzi wa tawi la Iyumbu Ernest Mahodanga aliyeusimamia uchaguzi huo, alimtangaza Nasson Mwibara kuwa ndiye aliyeongoza katika kura hizo za maoni katika nafasi ya mwenyekiti kwa kuibuka na kura 75 baada ya kuwabwaga wapinzani wake George Makapi aliyemaliza muda wake kwa kupata Kura 62 ambapo Amani Shaban Babyato aliyepata kura 6 wakati Emmy Issa Silla akipata kura 2 kwa mtaa wa Iyumbu
Akitawatangaza waliyeoongoza katika mtaa wa UDOM kuwa ni Venas Mwibala aliyeibuka na kura 55 dhidi ya 52 za mpinzani wake wa karibu John Chipuza wakati Zebedayo Mazengo akiibuka na kura 11 huku Rista Lalusa akiambulia kura 6
(PICHA ZOTE NA JOHN BANDA)