KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Ally Hapi *(MNEC)* amehitimisha kampeni za chama hicho mkoani Mbeya kwa kuhimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024. Katika hotuba yake, Hapi alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji kwa masilahi mapana ya maendeleo yao.
Alieleza kuwa CCM imejipambanua kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, na maji chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan
Huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa na imani na viongozi wa CCM, akisema kwamba rekodi yao inaonyesha matokeo ya kweli na kujali maslahi ya wananchi.
Hapi pia alisisitiza kwamba wagombea wa CCM wana uwezo wa kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo na kuleta mabadiliko chanya kwa jamii,pamoja na kuhimiza wananchi kuchagua viongozi wenye sera na uwezo wa kuboresha maisha yao.
Aidha Hapi amemwelezea Rais Samia Suluhu Hassan kuwa ameonyesha uongozi wa kipekee tangu alipoingia madarakani mwaka 2021, akifanikisha miradi ya maendeleo katika nyanja mbalimbali za maendeleo, kiuchumi, na kisiasa akisimia ukuaji wa uchumi kupitia diplomasia ya uchumi, ambapo ameimarisha mahusiano ya kimataifa na kuvutia wawekezaji wakubwa pamoja na kuongeza idadi ya watalii kupitia filamu ya The Royal Tour, ametangaza vivutio vya utalii na uwekezaji wa Tanzania kimataifa, hatua iliyoleta ongezeko fursa za ajira.
Katika sekta ya miundombinu Hapi alisema serikali imefanikisha ujenzi wa miradi mingi ya maendeleo kama madarasa zaidi ya 21,000, barabara za lami, na upanuzi wa huduma za usafiri wa anga pamoja miradi ya reli kama SGR na maboresho katika Shirika la Ndege la ATCL imepewa kipaumbele.
Kwa upande wa Demokrasia na Utawala Bora Rais Samia amefanya juhudi za maridhiano ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na kukutana na viongozi wa upinzani kama Freeman Mbowe hii imeonyesha nia ya kulinda demokrasia na kutafuta amani ya kitaifa.
Kwenye Huduma za Kijamii ameboresha huduma za afya na elimu kwa kuongeza bajeti, ajira kwa watumishi wa umma, na kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani kupitia ujenzi wa madarasa mapya. Pia amehakikisha maendeleo katika sekta ya sanaa na michezo.
Ameendelea kuzungumzia kuhusu haki za Binadamu ambapo Serikali imeonyesha utayari wa kutatua changamoto za haki za binadamu, ikiwemo kufuta mashtaka dhidi ya baadhi ya viongozi wa dini waliokuwa kizuizini kwa muda.
*Imeandaliwa na Idara ya Oganaizesheni ya Jumuiya ya Wazazi Taifa*








