BANDA MEDIA BLOG

IWE MVUA IWE JUA WANACCM TUKAPIGE KURA

 

 ...................

NA JOHN BANDA, DODOMA

MWENYEKITI wa chama cha mapinduzi (CCM), Kata ya Iyumbu jijini Dodoma Sadik Mponyamili amewataka wanachama wa chama hicho kutobweteka badala yake Waamke wakapige kura bila kujali kutakuwa na mvua au jua siku hiyo.

Sadik ameutoa Wito huo kwenye mkutano wa Kampeni za chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Mbuyuni Mtaa wa Nyerere, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kumnadi Ayoub Mandabaga anayegombea nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa huo Pamoja na wajumbe wa serikali ya mtaa.

“ kumekucha tuamke tukapige kura, siku ya uchaguzi itakuwa ni jumatano ndugu zangu wa mtaa wa Nyerere tuliojiandikisha tukapige kura kuchagua wagombea wa CCM, bila kujali kutakuwa na mvua au jua siku hiyo hakuna kulala kama kupanda tukapande alhamis”, amesema

Ayoub Mandabaga Mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyerere amejivunia, Usambazaji wa Umeme kwa asilimia 100, maji asilimi 80, ufunguzi wa mtaa kwa miundombinu ya Barabara, kamati ya maafa ambayo kwa sasa ina vyombo vya kuhudumia kwenye matukio lakini pia kuunda vikundi vya ujasiliamali kwa ajili ya kuchangamkia fedha za Rais Dkt. Samia Suluhu..

“katika kipindi cha miaka 5 iliyopita najivunia usambazaji wa maji, umeme, barabara na kamati imara ya maafa naombeni kura zenu nikaendelee kuwaletea maendeleo wakazi wa mtaa wa Nyerere kwa nina uwezo huo”, amesema

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Kata ya Iyumbu Luka Chipanga amewaomba waumini wa Dini mbalimbali, kumwomba Mungu ili kusitokee umauti kwa mpiga kura yoyote katika kata hiyo kabla ya siku ya uchaguzi na kwamba ili ujenzi wowote uwe Madhubuti lazima ufanyike hatua kwa hatua hivyo wagombea hao wapewe kura ili wakaendeleze walipoishia.


Vigogo wa CCM, Kata ya Iyumbu Mwenyekiti Mponyamili na Katibu wake Masai wakiteta jambo kwenye Mkutano huo wa kampeni kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa Nov 27,mwaka huu.

Mwenezi wa CCM, Kata ya Iyumbu akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na wanaccm kwenye mkutano huo wa kampeni








Elias Sutuchi (KING), Diwani wa kata ya Iyumbu akiongea jambo kwenye mkutano huo wa kampeni kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG