BANDA MEDIA BLOG

RAID DKT. MWINYI AREJEA ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zimbabwe na kurejea Zanzibar,Tanzania tarehe 21 Nov 2024.

 Katika  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe  Rais Dk, Mwinyi akiwa ameambatana na Mama Mariam Mwinyi na Ujumbe wake alipokelewa kiwanjani hapo na Mwanasheria Mkuu wa Zimbabwe Mheshimiwa Virginia Mabhiza na viongozi mbalimbali wa nchini humo pamoja na Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Simon Nyakoro Sirro.

Akiwasili uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar Rais Dk.Mwinyi alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali,vyama vya Siasa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdullah.

Rais Dk, Mwinyi katika Mkutano uliomalizika jana alimwakilisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk, Samia Suluhu Hassan ambae ni Mwenyekiti wa asasi ya Siasa,Ulinzi na Ushirikiano wa Usalama wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika [SADC].




 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG