"Gen S ni Program yenye lengo la kuwakutanisha vijana wote wa Kitanzania katika nyanja tofauti. Gen S ni Program ambayo imetohoa Jina lake kutoka Maneno Generation - Gen na neno Success ambayo inasimama kama S. Kauli ya mchagizo ya Gen S ni KIZAZI CHA MAFANIKIO. Na Kwa msingi huo wa Gen S kama kizazi Cha Mafanikio, tunaamini pia vijana wote wanaofanya Shughuli zao za kujitafuta katika nyanja mbalimbali kama ujasiriamali, wafanyabiashara, wanamichezo, maafisa usafirishaji na wajenzi wanaweza kuwa sehemu ya program hii ya Gen S." Hayo yamesemwa na Msemaji Wa Gen S Sonatta Nduka
Aidha Gen S inaamini katika Juhudi na mazingira rafiki yaliyowekwa na serikali ya Dkt Samia katika kuhakikisha vijana wanafanikiwa katika kipindi chake, hivyo tunaichukulia Gen S kama Generation Samia.
Gen S Ina lengo la kuwaconnect vijana na Fursa mbalimbali, kuonyesha mafanikio yao na kuwatafutia njia za mafanikio zaidi.
Kwa kulizingatia Hilo tumeona tuwaletee tukio kubwa la kuwaunganisha vijana kutoka Makundi mbalimbali kupitia GEN S JOGGING itakayofanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 07-12-2024 katika uwanja wa Jamhuri kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 3 asubuhi. Tunataraji kuwa na vijana kutoka sekta mbalimbali kama vikundi vyote vya jogging vya Dodoma, Umoja wa wafanyabiashara, wafanyakazi sekta binafsi na serikali. Tutaunganisha Makundi yote Kwa lengo Moja la kujenga Network yenye manufaa Kwa vijana.
"Hivyo nichukue nafasi hii kutangaza Rasmi kuwaalika wadau wote wa mazoezi na masuala ya vijana kushiriki nasi siku hiyo. Tunaamini Mbio hizi zitakuwa sehemu ya Mtoko Kwa wajanja wote wa Mjini, zitakuwa sehemu ya kujenga Network Kwa vijana mbalimbali, lkn kubwa kuliko itakuwa sehemu ya kujenga familia imara na kubwa ya Gen S."
Sonnata Nduka
Msemaji Gen - S
#Gen-S
#KizaziChaMafanikio
