BANDA MEDIA BLOG

WANAOHARIBU MIUNDOMBINU YA BARABARA CHINYOYO WAPIGWA MARUFUKU

 


NA JOHN BANDA, DODOMA

Mwenyekiti wa mtaa wa chinyoyo kata ya kilimani jijini Dodoma Faustina Bendera amewaonya wananchi kuacha tabia ya kukusanya na kusomba mchanga pebezoni mwa barabara za mtaa huo la sivyo watachukuliwa hatua kali ikiwemo kufikishwa mahakamai

Bendera ametoa onyo hilo baada ya kuona baadhi ya wanachi wakichota mchanga baada ya mvua kuanza kunyesha hivi karibuni, huku wakisababisha uharibiu wa miundombinu ya barabara hizo.

"Hivi karibuni baada ya mvua kunyesha kuna wananchi wameanza tabia ya kukusanya malundo ya mchanga katika barabara za mtaa Sasa ninawaambia ni marufuku kumwona mwananchi yoyote akisomba mchanga katika barabara za mtaa na yoyote tutakaye mkamata na kumchukulia hatua kali za kisheria ikiwa kupigwa fani na kupelekwa mahakamani"amesema Mwenyekiti Faustina

Aidha Mwenyekiti huyo amesema wanaotaka kusomba mchanga waende kwenye mtaro mkubwa unaujulikana kama mtaro wa wizara ya afya kwakuwa kuna mchanga unaoletwa na maji ya mvua pia watakuwa wamesaidia kuusafisha mtaro huo.

Mbalimbali na hilo mwenyekiti Faustina amewataadharisha wananchi katika kipindi hichi cha masika kuhakikisha wanafanya usafi katika maeneo yao ya nyumbani na mtaani ili kuhakikisha wanaepukana na magonjwa ya kuharisha (kipindupindu) ambacho kwa tarifa zilizopita tayari kimeshabisha hodi jijini Dodoma naekusababiaha vifo.

 

Aidha Mwenyekiti huyo amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu ya barabara zote za mtaa na kuwa wanatoa taarifa za maafa yoyote yatakayokuwa yanatokana na mvua hizi zinazoendelea kunyesha hapa Jiji Dodoma.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG