BANDA MEDIA BLOG

DOREFA YATANGAZA MAFANIKIO YA MWAKA 2024 KATIKA MICHEZO


Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kimetaja mafanikio iliyoyapata mwaka  2024 huku kikitoa  shukrani za dhati kwa wadau wote na familia ya mpira wa miguu kwa kuendelea kuungwa mkono katika kuendeleza michezo.

Mwenyekiti wa FA Dodoma Aden Mohammed kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya Chama hicho ameyataja mafanikio hayo ni pamoja na kuendesha Ligi za Vijana Dorefa U-17 League, Dorefa U-20 Youth League. Kuwa Mwenyeji wa Fainali za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa iliyotimua vumbi kuanzia tar 7-14 April, 2024. Kupandisha Timu ya Gunners FC kwenda First League(Ligi Daraja la Pili) huku FA ikitoa zawadi ya Shilingi milioni Moja kama motisha kwao.

Pia,Dorefa inajivunia Kuendesha Kozi mbalimbali za kiufundi kwa kushirikiana na TAFCA Mkoa wa Dodoma na TFF kupitia Mkurugenzi wa Ufundi Ndg.Oscar Milambo kama vile, Kozi nne za Diploma C (2020-2024), Kozi ya awali ya Grassroots iliyofanyika Mwezi Juni 2024 na CAF Diploma B iliyoanza hivi karibuni. 

Aidha mwaka 2024 Dorefa imefanikiwa kugawa vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya kuendeleza mchezo huo hasa maeneo yenye uhitaji mkubwa.

Hata hivyo Dorefa imeendelea kushirikiana na Wadau mbalimbali katika kuendeleza mchezo huu kwa kushiriki kikamilifu kama vile Michuano ya Ujirani Mwema Mavunde Ndondo Cup, Clouds Mavunde Ndondo Cup na mingine

Aidha,Mwenyekiti ametoa  shukrani za dhati kwa wadau wote na familia ya mpira wa miguu kwa kuendelea kuungwa mkono katika kuendeleza michezo.

"Kama Dorefa tunasema asanteni kwa ushirikiano mliotuonesha ahadi yetu ni kuendelea kushirikiana nanyi kuhakikisha Mkoa wa Dodoma unazidi kupaa katika maendeleo,"

"Mwenyekiti anawatakia  Mwaka Mpya mwema 2025  wenye mafanikio zaidi katika michezo Wadau wote hususani wa mpira wa miguu.

Imetolewa na :-

Idara ya Habari na Mwasiliano - DOREFA

08/01/2025 .

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG