BANDA MEDIA BLOG

HUDUMA YA 2=1 KUZINOA NDOA ZA WATANZANIA KUANZIA FEBRUARY 6 MWAKA HUU

 

Gavin na Ametia Moses ambao ni Wakurugenzi wa 2=1 Kanda ya Africa  wanatarajiwa kutua nchini February 6,2026

WAKURUGENZI wa kanda ya Afrika wa Huduma ya mbili sawa na moja (2=1) yaani kwa kimombo 2 EQUAL 1, Gavin na Ametia Moses, wanatarajiwa kutua nchini Tanzania kuanzia Feb 6, mwaka huu kwa Ziara ya semina ya wanandoa kupitia neno la Mungu.

Mwenyekiti wa Mkoa wa Dodoma na mjumbe wa Taifa wa 2=1, Askofu Dkt. Eliah Mauza amenukuliwa na Tv ya mtandaoni ya BANDA MEDIA, kuwa wakurugenzi hao ambao ni mke na Mume watatua nchini wakitokea Nchini Afrika ya kusini ambapo Ziara yao itaanzia jijini Mwanza, Katavi na kisha Dodoma.

“kwa kuwa semina yenyewe ni ya wanandoa, wakurugenzi hao pia ni mke na mume, wanakuja kuleta semina ya kuziponya na kuziimarisha ndoa zetu, kwa kupitia vikundi vya watu 15 ambao watakuwa mume na mke hivyo kukamilisha idadi ya 30 (power house)”, amesema

Aidha Dkt. Mauza  akifafanua zaidi amesema baada ya wageni hao kuingia hapa nchini kwa ziara ya siku 7, wataanzia jijini Mwanza kati ya feb 7 hadi 9, Katavi feb 11 hadi 12 na kisha Dodoma kwa siku mbili za Feb 14 na 15, 2026 katika kanisa la PRA, ambapo ziara hiyo itakamilishwa rasmi.

Amesema kuhusu mapokezi ya wageni hao maandalizi kwa upande wa Dodoma yanaendelea nzuri, huku akiwahimiza wajumbe wa kamati ya mapokezi kuendelea kujidhatiti kwani siku hazisimami..

Ameongeza kuwa awali vikundi (POWER HOUSE) vyolivyokuwa vimeundwa mkoani Dodoma vitahuwishwa huku vingine vipya vikianzishwa, ambavyo vitawahusisha wanandoa wenyewe, wanaotarajiwa kuingia katika Ndoa wakiwemo wajane, na kwamba semina hiyo haibagui Dini wala dhehebu la mtu.

Ikumbwe kuwa 2=1 ni chuo kuu cha Ndoa, ambacho kimesambaa kutoa huduma kwa wanandoa, Ulimwenguni kote kikianzishwa  nchini Australia, msisitizo ukiwa kwa watakaofaulu na kuyaishi mafunzo hayo wataanzishiwa Miradi huduma hiyo…

kumradhi Mabadiliko ya Majina ya Wakurugenzi hao, yanatokana na kukosewa hapo awali..

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG