BANDA MEDIA BLOG

WANANCHI NA WATALII WAIPA CONGOLE SEKTA YA MADINI, KWENYE MAONYESHO YA BIASHARA ZANZIBAR

 

📍 Zanzibar 

Wananchi na watalii waliotembelea Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar yanayoendelea Fumba wameonesha kuvutiwa na fursa mbalimbali za uwekezaji zinazotolewa na Sekta ya Madini, hususan katika maeneo ya utafiti, uchimbaji mdogo, uchenjuaji, uongezaji thamani na biashara ya madini.

Wametembelea Banda la Tume ya Madini kujifunza taratibu za kujiandikisha, kuomba leseni za uchimbaji mdogo (PML), pamoja na kupata ushauri wa kitaalam kuhusu namna ya kushiriki kikamilifu katika sekta hiyo inayokua kwa kasi na kuchangia ajira, kipato na maendeleo ya uchumi wa nchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG