Mvutano umeendelea kufuatia mchezo wa Nusu Fainali ya Michuano ya Africa U-17 Cup of Nations kati ya Morocco na Senegal,
Baada ya kuibuka kwa Taarifa zinazodai kuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Morocco,
Fouzi Lekjaa, anapanga kuwasilisha Malalamiko rasmi kwa CAF.
Kwa mujibu wa Taarifa mbalimbali zinazo sambaa, upande wa Morocco unadaiwa kutaka Penalti moja iliyopigwa kwenye Mchezo huo irudiwe, wakieleza kuwa kulikuwa na Mchezaji wa Morocco aliyeingia ndani ya eneo la Mita 18 kabla ya mpira kupigwa,
Jambo ambalo limezua mjadala mkubwa kuhusu tafsiri ya Sheria za Mchezo.
Tukio hilo limeibua Mjadala mkali kwenye Mitandao ya Kijamii, huku Mashabiki wa Soka kutoka Mataifa mbalimbali wakitoa Maoni tofauti kuhusu Uamuzi huo pamoja na uwezekano wa CAF kuchukua hatua yoyote rasmi.
Katika Mchezo huo, Senegal walifanikiwa kuibuka na Ushindi wa Penalti 7-6 baada ya Timu hizo kutoka Sare ya 1-1 ndani ya
Dakika 90 za kawaida, na sasa wamefanikiwa kufuzu kwenda Fainali ambapo watakutana na 🇹🇿 Tanzania. 🇹🇿
Hadi sasa, CAF bado haijatoa Taarifa rasmi kuhusu uwepo wa malalamiko hayo au hatua yoyote inayoweza kuchukuliwa.
