BANDA MEDIA BLOG

CHUO KIKUU ST JOHN’S CHAANDAA VIJANA WENYE MAARIFA WANAOZINGATIA MAADILI YA KITANZANIA

Na Maiko Luoga  – Dodoma

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha St John’s kilichopo chini ya Kanisa Anglikana Tanzania (St John’s University of Tanzania – Dodoma) Lay. Can. Profesa Yohana Msanjila, ametoa wito, kwa wanafunzi kujiunga na chuo hicho ili kupata Elimu ya juu inayotolewa chuoni hapo.

Prof. Msanjila ameutoa wito huo wakati akizungumza kwenye Ibada ya Misa Takatifu ya Kipaimara, iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Stephano Kikuyu jijini Dodoma, ambapo ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu Dickson Chilongani wa Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) ambaye pia ni Mkuu wa Chuo hicho. 

“Nactevet, wametoa matangazo ya kujiunga na Elimu ya Vyuo Vikuu, Chuo chetu Kikuu cha St. John’s kinapokea wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na Kidato cha sita, Chuo kinatoa Diploma (Astashahada) na Cheti, katika kozi mbalimbali, Tutumie nafasi hii kujiunga na Chuo Kikuu cha St John”s” Amesema Prof. Msanjila. 

kwa upande wake Askofu wa DCT. Dickson Chilongani ambaye pia ni Makamu wa Askofu Mkuu (Dean) Kanisa Anglikana Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, ametumia nafasi hiyo kuwalika watanzania na watu wote kutumia fursa ya kupata Elimu ya juu katika chuo hicho.

“Tuwaalike watu wote nchini, kuja kujiunga na Chuo Kikuu cha St John’s Hapa Dodoma ili kupata Elimu bora yenye vigezo kamili na kuzingatia maadili ya Kitanzania, Tuandae vijana wenye maarifa ili waje kulitumikia Taifa letu” amesema Askofu Chilongani (Dean).

Taarifa za mawasiliano, St John’s University of Tanzania, P.O. Box 47, Dodoma, Tanzania. | Email: admissions@sjut.ac.tz Mobile: +255 712 882 734, 0754 285 909 | Website: www.sjut.ac.tz.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG