BANDA MEDIA BLOG

MBUNGE MAVUNDE AWEZESHA VIJANA JIMBO LA MTUMBA PIKIPIKI 50

 

*JIMBO LA MTUMBA*

ZAIDI ya pikipiki 50 tayari zimegawiwa kwa vikundi mbalimbali vya vijana wa jimbo la Mtumba, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza ajira, kukuza kipato na kuimarisha ushiriki wa vijana katika shughuli za maendeleo.
hayo yamesemwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya CCM (UVCCM), Shabani Shabani ambapo amesema program hiyo itawakwamua vijana kiuchumi.

"Hatua hii inaonesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha vijana wanapata fursa za kujitegemea kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa letu", amesema

Aidha CDE Shabani amemshukuru Mbunge wa jimbo hilo Anthony Mavunde  kwa kuendelea kuweka mbele maslahi ya vijana na kutekeleza kwa vitendo falsafa ya "Kazi na Utu, Tunasonga Mbele."
Vijana ni nguvu kazi ya Taifa; tukiwawezesha vijana, tunajenga Tanzania imara na lenye maendeleo endelevu.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG