BANDA MEDIA BLOG

RAIS, DKT. SAMIA AMEDHAMIRIA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

MKIMBIZA  Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwang’onda amewaambia wananchi wa Wilaya ya Dodoma  kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuwainua vijana kiuchumi na fursa zinaendelea kuja nyingi kwao.

Alizungumza hayo leo tarehe 1/6/2026 baada ya kupokea taarifa kutoka Kikundi cha Mwamko wa Vijana Kiuchumi ambao ni miongoni mwa miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2026 wilayani Dodoma chini ya kaulimbiu isemayo ‘Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo’.

“Mkuu wa Wilaya ya Dodoma nikushukuru sana kwa kazi nzuri ya kusimamia vijana hawa kupata mkopo, lakini nataka niwaambie vijana wenzangu kwamba Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kutuinua kiuchumi na fursa nyingi zinakuja. Anachokiomba yeye kutoka kwenu ni kuendelea kulinda amani ya Jiji la Dodoma na Tanzania kwa ujumla na viongozi wote wapo tayari kututumikia wa Tanzania”alisema Mwang’onda.

 MWISHO





 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG