Alves, ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za Barcelona, Juventus na Paris Saint-Germain (PSG), amekuwa akionekana akihubiri katika mikutano na ibada mbalimbali, akitoa ushuhuda wa mabadiliko aliyopitia maishani mwake. Ripoti mbalimbali zimeonyesha kuwa amekuwa akihudhuria na kushiriki katika makanisa ya kiinjili, akisema kuwa alifanya “agano na Mungu” na sasa analenga kuitangaza Injili. (CNN Brasil)
Safari yake ya kiroho ilikuja baada ya kupitia kipindi kigumu kufuatia kushikiliwa na kufungwa nchini Hispania kuhusiana na kesi iliyomkabili. Baada ya kuachiwa kutoka gerezani na baadaye kuanza maisha mapya, Alves aliamua kuelekeza nguvu zake katika imani na huduma ya Mungu. (Reuters)
Mabadiliko hayo yamezua mijadala mitandaoni, huku baadhi ya watu wakiyasifu kama ushuhuda wa nguvu ya mabadiliko kupitia imani, na wengine wakisisitiza kuwa kila mtu anapaswa kuwajibika kwa matendo yake pamoja na kuheshimu mchakato wa haki.
