BANDA MEDIA BLOG

Baraza la Usalama la UN kutuma wanajeshi Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatazamiwa hii leo kuidhinisha kwa kauli moja azimio lililoandaliwa na Ufaransa linalonuia kuhitimisha mgogoro wa kisiasa nchini Burundi. Iwapo azimio hilo litapasishwa, basi Umoja wa Mataifa utaanzisha mchakato wa kutuma vikosi vya kulinda amani katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Kadhalika azimio hilo linapendekeza kuwekewa vikwazo shakhsia wa kisiasa wanaochechea machafuko nchini humo. Duru za kidiplomasia za Ufaransa zimeeleza matumaini yao kuwa azimio hilo litaungwa mkono na wananchama wote 15 wa Baraza la Usalama. Zaidi ya watu 240 wameuawa huku wengine zaidi ya laki 2 wakilazimika kuitoroka nchi na kuwa wakimbizi katika nchi jirani, tangu machafuko yaanze nchi Burundi mwezi Aprili mwaka huu. Machafuko hayo yalianza baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kutangaza azma yake ya kuwania urais kwa muhula wa tatu, hatua ambayo wapinzani nchini humo wanashikilia kuwa ilikiuka katiba ya nchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG