BANDA MEDIA BLOG

CRISTIANO RONALDO AZINDUA FILAMU YAKE JIJINI LONDON


Filamu fupi ya nyota wa soka duniani Cristiano Ronaldo imezinduliwa Jijini London huku Sir Alex Ferguson akijiunga na mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United katika uzinduzi huo uliofanyika jana jioni.

Mchezaji huyo wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 30 alikuwa huko Leicester Square Uingereza kuangalia kwa mara ya kwanza filamu hiyo fupi iliyoongozwa na James Gay-Rees
na kupatiwa jina la 'Ronaldo'.

Filamu hiyo fupi imetengenezwa kwa miezi 14, wakati Ronaldo akishinda Kombe Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na Real Madrid mwaka 2014. Jose Mourinho, Carlo Ancelotti, Radamel Falcao, Gary Neville pamoja na Louis Saha walihudhuria pia uzinduzi huo.
Ronaldo akiwa na kocha Carlo Ancelotti na wakala Jorge Mendes
  Kocha Jose Mourinho akiingia ukumbini kuangalia filamu hiyo
Ronaldo akiwa na Sir Alex Ferguson

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG