Diwani mteule wa Kata ya Chamwino Ikulu Julius Maguwo (kulia)akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa afisa mtendaji wa Kata hiyo,Adrego Asanga (kushoto)jana katika ofisi za afisa Mtendaji wa Kata hiyo. Picha na Ramadhan Hassan
Na John Banda,CHAMWINO
DIWANI
Mteule wa Kata ya Chamwino Ikulu,Julius Maguwo(CCM) amemkaribisha Rais mteule Dk
John Magufuli katika ikulu ya Chamwino Dodoma kwa ajili ya mapumziko kutokana na
hekaheka za uchaguzi.
![]() |
| Diwani mteule wa Kata ya Chamwino Ikulu (CCM)Julius Maguwo akionesha cheti cha ushindi mara baada ya kukabidhiwa jana katika ofisi ya afisa Mtendaji. |
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada
ya kukabidhiwa cheti cha ushindi na Msimamizi wa uchaguzi katika Kata hiyo,Asanga
Adrego,Maguwo alisema pamoja na kuchaguliwa ni jukumu lake kuhakikisha Rais
anakuwa katika mikono salama kutokana na eneo lake kuwa Ikulu.
‘’Hapa ni
Ikulu hivyo kutokana na mikimiki ya uchaguzi namwomba Dk Magufuli aje apumzike
namwaahidi atakuwa sehemu salama na yenye utulivu,kwani hata Mwalimu
Nyerere,Jakaya Kikwete na Benjamini Mkapa wameitumia sana hii Ikulu’’
Pia Maguwo aliahidi kutekeleza kwa viendo
ahadi yake aliyoihaidi ya kuhakikisha Kata hiyo inakuwa na maji safi na salama
katika kipindi chake ambacho atakuwa madarakani.
Maguwo alisema
pia atahakikisha katika Kata hiyo madawati yanapatikana katika shule pamoja na
kuzitatua changamoto zote zinazohusu maendeleo.
Tags
HABARI KITAIFA

