 |
| Hapa
ni katika ukumbi wa Flomi Hotel mjini Morogoro ambako leo Ijumaa
Novemba 06,2015 kunafanyika mkutano mkuu wa wanachama wa Muungano wa
Klabu za waandishi wa habari Tanzania-UTPC wanakutana kujadili mambo
mbali mbali ili kuboresha taaluma ya uandishi wa habari nchini
Tanzania.Mkutano huo wa siku mbili unakutanisha wenyeviti wa klabu za
waandishi wa habari Tanzania,makatibu na waweka hazina.Katika mkutano
huo pia utafanyika uchaguzi wa rais wa UTPC na wajumbe wa bodi wa
UTPC-Fuatilia picha hapa chini kinachoendelea ukumbini-Picha zote na
Kadama Malunde na Shomari Binda-Malunde1 blog. |
 |