BANDA MEDIA BLOG

MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA VITI, VITANDA NA MACHELA


Viti vilivyotolewa na kampuni hiyo.
Dk Mfinanga akipokea msaada huo leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

 Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Matangazo ya Ashton Media akiwapatia maji wagonjwa waliolazwa kwenye jengo la Sewahaji katika hospitali hiyo.
…………………………………..
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), leo imepokea msaada wa viti vitano kwa ajili ya shughuli za utoaji damu, vitanda vitano vya kuzalisha kina mama na machela tano za kubebea wagonjwa mahututi.
Msaada huo umepokelewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga wa hospitali hiyo.
Akizungumza katika tukio hilo, Aligaesha ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo kwa kuwa utasaidia kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
“Kampuni hii imetupatia msaada mkubwa kwani ni moja ya msaada tuliokuwa tunauhitaji sana,” amesema Aligaesha.
Naye Dk Mfinanga amesema machela zilizotolewa zitasaidia kubeba wagonjwa mahututi na kuwapeleka kwenye kitengo hicho kwa ajili ya kupatiwa huduma kwa wakati na kuokoa maisha ya wagonjwa

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG