 |
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues
(katikati) akisalimiana na Mjumbe wa bodi udhamini ya Mtandao wa Radio
Jamii Tanzania (COMNETA), Balozi Mstaafu, Christopher Liundi alipowasili
katika mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa
waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa
habari na uandishi unaozingatia maadili ulioandaliwa na UNESCO. Kulia
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof.
Ole Sante Gabriel.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Serikali
mpya ya awamu ya tano iliyochini ya rais Dr. John Magufuli, imeahidi
kushirikiana na mashirika na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakipambana
kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa salama na kufanya kazi zao kwa
uhuru bili kuingiliwa ufanyaji wa kazi zao na mtu yoyote.
Ahadi
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Prof. Ole Sante Gabriel katika mkutano wa kitaifa wa
mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa
kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia
maadili ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia na
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Prof. Gabriel amesema
serikali ya awamu ya tano ipo tayari kushirikiana na mashirika na wadau
mbalimbali ambao wapo kuwasaidia waandishi wa habari ili haki zao ziweze
kutekelezwa kutokana na kuwepo kwa uvunjaji wa haki za wanahabari.
Amesema
wanatambua kuwepo kwa changamoto hizo kwa waandishi wa habari na kwa
serikali ya awamu ya tano itahakikisha kushirikiana na mashirika na
wadau ili kutetea haki za wanahabari kwa kuwa na uhuru katika utendaji
wa kazi zao bila kuingiliwa na mtu.
“Naahidi
kuanzia sasa serikali itakuwa ikishirikiana nanyi kusaidia kuhakikisha
kunakuwa na uhuru wa vyombo vya habari, nchi yetu kwa sasa haina sababu
ya kuacha kuungana na ninyi kutokomeza vitendo hivyo kwa wanahabari,
serikali ni mpya na tutalitekeleza jambo hilo kila tumaposhirikishwa
kuhusu vitendo vibaya kwa wanahabari,” amesema Prof. Gabriel.
|

kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
kufungua.
Aidha
Katibu Mkuu huyo amewata waandishi wa habari kuwa pamoja na usaidizi
ambao wizara imeamua kujitoa kuwasaidia pia wanapaswa kuandika habari
zenye weledi na zilizo sahihi kwani kumekuwepo na kundi kubwa la
waandishi wa habari ambao wamekuwa wakiandika habari ambazo hazina
uhakika wala weledi na hivyo kuupotosha umma kwa habari wanazoandika ila
kuanzia sasa wanabidi kubadilika kwa kuandika habari ambazo zitakuwa na
fadia kwa jamii inayowazunguka.
Kwa
upande wa UNESCO, kupitia kwa Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
nchini, Zulmira Rodrigues, amesema kumekuwepo na vitendo vingi ambavyo
sio vya kibinadamu ambavyo wamekuwa wakifanyiwa waandishi wa habari na
wao wameamua kujitoa kuhakikisha wanatokomeza vitendo hivyo.
Amesema
kama jamii ikiungana kwa pamoja kutokomeza vitendo hivyo inawezekana
kwani kutokuwepo uhuru wa waandishi wa habari katika utendaji wao wa
kazi kunapelekea jamii kukosa baadhi ya taarifa muhimu ambazo kama
kukipatikana uhuru wa habari kutawapa fursa wanahabari wa kuzitoa
taarifa hizo.

 |
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Ole Sante
Gabriel akisisitiza jambo wakati akifungua rasmi mkutano wa kitaifa wa
mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa
kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia
maadili ambao umeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na
Elimu, Sayansi (UNESCO).
“UNESCO
tunapenda kuona vitendo hivyo havifanyiki kwa waandishi wa habari kama
kuweka sheria ambazo zinawabana na kusababisha wanashindwa kufanya kazi
zao kwa uhuru na tunaweza kuona kama serikali na kila mtu akiwa tayari
tunaweza kumaliza tatizo hilo,” amesema Rodrigues.
Nae
Makamu wa Rais wa Chama cha Kijamii cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS),
Flaviana Charles amesema imekuwa ngumu kesi zinazokuwa zikiwahusu
waandishi wa habari juu ya vitendo vya kikatili wanavyotendewa kutokana
na ucheleweshwaji wa upelelezi unaofanywa na Jeshi la Polisi Tanzania
akitolea mfano kesi ya mwandishi wa zamani wa Chaneli 10 mkoani Iringa,
Daudi Mwangosi ambapo mpaka sasa ina miaka 4 na bado upelelezi
haujakamilika.
|



Kutoka kushoto ni Ofisa miradi
katika kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizilege,
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),
Mwanasheria Onesmo Olengurumwa, Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
nchini, Zulmira Rodrigues pamoja na Makamu wa Rais wa Chama cha Kijamii
cha Wanasheria wa Tanganyika, Bi. Flaviana Charles katika picha ya
ukumbusho.
 |
| Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Ole Sante Gabriel (kushoto)
akifurahi jambo na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville
Meena mara baada ya zoezi la picha ya pamoja. |
Ofisa Miradi katika kitengo cha
Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizilege akiwasilisha mada ya
Uhuru wa vyombo vya Habari katika mkutano huo.
 |
| Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM) katika tasnia ya Habari na Mawasiliano, Ayub Rioba
akiwasilisha mada ya wajibu wa vyombo vya habari huku akitolea mfano wa
moja ya habari iliyobeba kichwa cha habari “Uhuru wa habari watikiswa
Zimbabwe” katika moja ya magazeti ya Serikali wakati wa mkutano wa
kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari,
uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi
unaozingatia maadili ulioandaliwa na UNESCO. |
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi
wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Mwanasheria Onesmo Olengurumwa
akielezea jinsi mtandao wake unavyotoa msaada kwa wanahabari wanaokumbwa
matukio mbalimbali katika utendaji wao hususan msaada wa kisheria.
 |
| Mhariri Mtendaji wa Gazeti la
Tanzania Daima, Neville Meena akiuliza swali kwa Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (MAELEZO), Assah Mwambene (hayupo pichani) katika mkutano wa
kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari,
uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi
unaozingatia maadili sambamba na kuadhimisha “International Day to
#EndImpunity” ulioandaliwa na UNESCO. |
 |
| Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Assah Mwambene akitolea ufafanuzi wa swali la Mhariri
Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena (hayupo pichani). |
 |
| Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akitoa maoni katika katika mkutano wa
kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari,
uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi
unaozingatia maadili sambamba na kuadhimisha “International Day to
#EndImpunity” ulioandaliwa na UNESCO. |
Mwandishi wa habari mkongwe, Halima Sharrif akitoa maoni katika mkutano huo.