BANDA MEDIA BLOG

Wachezaji wa zamani wa timu za Taifa Bara na Z’bar kucheza mchezo maalum.


Wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na wachezaji wa zamani wa timu ya Zanzibar Heroes watacheza mechi ya kirafiki December 09 mwaka huu kwa Lengo la kuhamasisha amani katika visiwani Zanzibar.
Mechi hiyo itapigwa katika Uwanja wa Amani ambapo pande zinazotofautiana kisiasa zitaalikwa ili kuzungumza na wanachama kuwa watulivu kipindi hiki ambapo suluhu inatafutwa.

Wakati huohuo michuano ya kuwania kombe la Challenge inaendelea huko nchini Ethiopia,timu ya Kilimnajaro Stars imeanza vyema baada ya kuibebesha mzigo wa mabao 4-0 Somalia.
Mabao ya timu hiyo kutoka Tanzania Bara yamefungwa na John Boko aliyefunga mawili sawa  na Elias Maguli.
Kilimanjaro Stars iliyopo kundi A itashuka dimbani siku ya jumanne kutoana jasho na timu ngumu ya Rwanda
Kukiwa bado kuna sintofahamu ya kisiasa visiwani Zanzibar njia mbalimbali zinatumika kumaliza sintofahamu hiyo ambapo sasa mchezo wa mpira wa miguuu nao unajitosa kuokoa amani ya visiwa hivyo.
Mechi hiyo inaratibiwa na mchezaji wa zamani wa Zanzibar Heroes Abdallah Maulid akishirikiana na wachezaji wa zamani Taifa Stars Lawrance Mwalusako pamoja na kitwana Manara Popat.
Hii si mara ya kwanza kwa soka kutumika kuhamasisha amani mwaka 2007 Nchini Ivory Coast yakifanyika mashindano ya CHAN na Shirikisho la soka barani Afrika lilieleza kuwa limeamua kupeleka mashindano hayo nchini humo ili kuwaleta pamoja wananchi wa eneo baada ya kutofautiana katika mambo ya Siasa.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG