Tukio la mafuriko makubwa katika
Jiji la Nairobi limeonekana kudhibitiwa kiasi lakini kupasuka kwa
mifumo ya maji taka na maji yake kuingia kwenye mito kumeanza kuzua
hofu kwa wakazi wa Jiji hilo.
Kuonekana kuzagaa kwa maji taka
kumeonekana kuwa ni jambo la kawaida baada ya mifumo ya kupitishia
maji taka kuvunjika na kutoboka kutokana na mvua kubwa zinazohusishwa
na El Nino.
Tags
KIMATAIFA
