Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile na Balozi
wa Japani nchini Bw. Masaharu Yoshida wakibadilishana hati ya mkataba wa
mkopo wa Shilingi Bilioni 210 kwa ajili ya mradi wa Umeme kati ya
Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile na Balozi wa Japani nchini Bw.Masaharu Yoshida wakisaini mkataba wa mkopo. Nyuma yao kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Omar Chambo, kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Seiji Kihara wakishuhudia tukio hilo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Jijini Dares Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi wa matumizi ya mkopo wa bilioni 210 baada ya kusaini mkataba wa mkopo huo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.

…………………………………………………………………………..
Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania imesaini mkataba na Serikali ya Japani kiasi cha shilingi
Bilioni 210 kwa ajili ya maendeleo ya mradi wa njia ya kusafirishia
umeme kati ya Tanzania na Kenya ambao utasaidia upatikanaji wa umeme wa
kutosha.
Mkataba huo wa masharti nafuu
ulisaininiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu
wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Balozi wa Japani nchini Tanzania
Bw. Masaharu Yoshida jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa
habari baada ya kusaini mkataba huo Dkt. Likwelile alisema kuwa fedha
hizo zitaelekezwa katika kusambaza nyaya za umeme zenye KV400, na urefu
wa kilometa 414.5 kati ya Singida na Namanga kupitia Babati na Arusha.
Alisema kuwa kukamilika kwa mradi
huo kutachochea maendeleo ya jamii na uchumi nchini kwa kuleta muungano
wa kibiashara katika nchi za Afrika Mashariki.
Naye Balozi wa Japani nchini
Tanzania Bw. Masaharu Yoshida alisema kuwa mkopo huo utafanikisha
kusambaza nyanya za umeme zenye urefu wa takribani kilometa 508 kati ya
Tanzania na Kenya ambapo Tanzania itasambaza kilometa 415 wakati Kenya
itakuwa na kilometa 93.
Japani imekuwa ikisaidia Tanzania
katika miradi ya umeme kwa muda mrefu, miradi ambayo tayari imekamilika
ni pamoja na usambazaji umeme Zanzibar, mradi wa usambazaji nyaya za
umeme mkoani Kilimanjaro na mradi wa kutengeneza nyaya mpya za umeme
jijini Dar es Saalam.
IMETOLEWA NA WIZARA YA FEDHA
KITENGO CHA MAWASILIANO
Tags
HABARI KITAIFA