BANDA MEDIA BLOG

PAPA FRANCIS AWATAKA WAKATOLIKI KUTOENDEKEZA KUJILIMBIKIZIA MALI MNO NA UBINAFSI

Papa Francis amewaonya waumini bilioni 1.2 wa kanisa hilo duniani kutokubali kuingiwa na sumu ya kupenda kujilimbikizia mali mno, katika ujumbe wake wa Krismasi.

Akiongea kwenye ibada ya mkesha wa Krismasi la Mtakatifu Peter, Basilica, Papa Francis amewataka waumini kuishi maisha ya kawaida yenye kuzingatia upendo, usawa na kusaidiana, ambayo si ya ubinafisi na kuongozwa na tamaa ya kujilimbikizia mali.

Baadae hii leo Papa Francis atatoa ujumbe wake wa Krismasi kama ilivyo kwa tamaduni za Kanasa Katoliki, akiwa eneo la balkoni eneo la kwenye uwanja wa Mtakatifu Peter.
Papa Francis akibusu mdoli wa mfano wa mtoto Yesu katika ibada kwenye kanisa la Mt. Peter, Basilica

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG