BANDA MEDIA BLOG

WAENDESHA BAJAJ MANISPAA YA DODOMA WAGOMA KWA SAA KADHAA, WAKISHINIKIZA WENZAO WALIOKAMATWA NA MANISPAA, KWA MADAI YA KUVUNJA SHERIA ZA BARABARANI WAACHIWE


Bajaj zikiwa nje ya jengo la Mhandisi wa manispaa ya Dodoma, Kutokana na wenye Bajaj hizo Kugoma kutoa huduma kwa Saa Kadhaa wakishinikiza kuachiwa kwa wenzao 12 waliokamatwa wakipakia abari katika Barabara ya NK, Kinyume cha Sheria.

Waendesha Bajaj katika manispaa ya Dodoma wakiwa wakitoa malalamiko yao mbele ya waandishi wa Habari nje ya jengo la mhandisi wa Manispaa ya Dodoma kutokana na Wenzao Kukamatwa wakidaiwa kuvunja Sheria za upakiaji Barabarani. [PICHA ZOTE NA BANDA BLOG]

Waendesha Bajaj hao wakijadiliana jambo

Kutokana na Kitendo hicho Ikamlazimu Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Clemens Mkusa afike kuwasikiliza na kisha kuwataka waendelee kutoa huduma wakati swala lao linashuhulikiwa
Kaimu Mkurugenzi huyo akiwatuliza waendesha Bajaji hao kabla ya kuzungumza nao
Baada ya mazungumzo hayo waendesha bajaj hao wakazunguka mtaa wa pili wa NK ambapo wenzao walikamtwa na kisha wakaendelea kupakia Abiria

Baadhi ya Madereva Tax wanaoegesha katika maeneo ya NK wakijadiliana jambo wakati wenye Bajaj walipokuwa wakiingia katika eneo hilo wakitokea Manispaa ambako shinikizo la kuwatetea wenzao halikufua Dafu



Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG