BANDA MEDIA BLOG

General News David Kafulila na kesi mpya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma….

Taarifa ninayokusogezea ni ya David Kafulila aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, tunafahamu ana kesi Mahakamani ya kupinga matokeo ya ubunge 2015 jimbo la Kigoma Kusini kesi ipo Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, taarifa ikufikie kuwa Kafulila baada ya kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma akasomewa kesi mpya ambayo anakiri hakuwa anaifahamu mwanzo kwenye sentensi zake; – David Kafulila
20150731001754
David Kafulila
Nilifikishwa mahakamani kwa kesi mpya ukiachilia kesi ya kwanza ya kupinga matokeo ya uchaguzi 2015 jimbo la Kigoma kusini, awali nilikuwa nikijua ninakesi moja katika mahakama ya hakimu mkazi kigoma kwa madai kwamba nilimdhalilisha aliyekuwa mkuu wa wilaya Khadija Nyembo tangu mwaka 2013….nikiwa mahakamani nikapewa tena kesi nyingine ni kesi ya kuhamasisha wananchi wasichangie mchango wa maabara; – David Kafulila
David-Kafulila1
Bado msimamo wagu utabaki palepale kwamba nitaendelea kupigania nchi yangu, kesi hizi zote katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma ukitazama hati za mashitaka yote ya Kafulila hapa Kigoma zimeandaliwa na kusainia na DPP makao makuu Dar es salam inawezekanaje;- Kafulila

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG