BANDA MEDIA BLOG

JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LATOA UFAFANUZI KUHUSU ALBINO ALIYEKUTWA KAFA



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP David A. Misime atoa ufafanuzi baada ya kutokea taharuki, maswali mengi na kuenea kwa uvumi mwingi kuwa KABURU RAMADHAN, mwenye Ualbino ameuwawa na watu wasiojulikana katika mtaa wa Mwausi Kata ya Majengo Wilaya ya Dodoma.

Askari Polisi wakiufanyia uchunguzi mwili wa Albono aliyekutwa kafa katika Mjengo Dodoma
Katika taarifa yake Kamanda Misime alisema; Leo tarehe 09.01.2016 majira ya saa 07:00 asubuhi tulipokea taarifa kuwa huko katika Mtaa wa Mwausi, Kata ya Majengo, Wilaya ya Dodoma kuna mtu mwenye Ualibino anaonekana ameuawa.


Baada ya kupokea taarifa hiyo nilifika katika eneo la tukio nikiwa na Afisa Upelelezi wa Mkoa na Wilaya pamoja na Wataalam wa Ukaguzi wa matukio ya kijinai.

Tulikuta mwili wa mwanaume mwenye ualibino na pembeni yake kukiwa na damu.

Baada ya Uchunguzi wetu wa awali wa kitaalam tuligundua mwili wake haukuwa na jeraha lolote lile na hana upungufu wa kiungo chochote. Kulingana na uchunguzi huo wa awali ambao tulishirikisha baadhi ya wana ndugu tulibaini damu iliyookuwa ikionekana ni matapishi yaliyochanganyikana na damu.

Mtu huyo kwa mujibu wa ndugu zake anaitwa KABURU S/O RAMADHANI, MIAKA 32, MNYAKYUSA, MKAZI WA KIKUYU KWA MAKBEL.
Ili Kujiridhisha zaidi na chanzo cha kifo chake mwili ulifanyiwa uchunguzi na Daktari na kutoa maoni yake ya kitaalam kuwa kifo chake kimechangiwa na mambo matatu:-
1.   VIDONDA VYA TUMBO – ambavyo vimeota usugu na kusababisha kuvuja kwa damu ndani ya tumbo (UPPER G1 BLEEDING)

2.   KUKOSA MAJI MWILINI – ambako kumesababishwa na kutapika kwa muda mrefu bila kupata msaada wa maji (HYPOVOLAEMIC SHOCK)

3.   KUKOSA HEWA: hii imetokana na kutapika akiwa amelala chali na kusababisha matapishi kuziba njia ya hewa.

Hivyo basi kwa mujibu wa Uchunguzi wa awali wa Polisi na wa Daktari ambaye kwa mujibu wa Sheria ndiye mwenye mamlaka ya kutoa maoni ya kitaalam nini chanzo cha kifo cha marehemu, kifo hicho hakikutokana na Mauaji kama ilivyoripotiwa awali au na uvumi unaoenezwa mitaani bali ni kifo cha kawaida kilichotokana na sababu nilizozieleza hapo awali.

Wito kwa wananchi wanapohisi ugonjwa wowote waende Hospitali ili wapate ushauri wa kitaalam utakaosaidia kupata tiba. Watu wasinywe pombe bila kula na kupita kiasi. Mwisho waepuke kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa na wataalam.


Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
(Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi - David Misime)





Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG