Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto)
akiwasili Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mtaa wa
Lumumba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kulia
ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba, kulia ni Mkuu
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha.
Katika hotuba yake, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa
kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kulia) akitoa taarifa ya
utendaji wa Jeshi lake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) wakati Katibu Mkuu huyo
alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es
Salaam. Katika hotuba yake, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa
utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji
wa mapato. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan
Simba. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na Makamanda
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Kamishna Jenerali, Pius
Nyambacha (wapili kulia) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara Makao
Makuu ya Jeshi hilo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo. Katika
hotuba yake, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi
mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato.
Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba.
Kulia ni Fikiri Salla, Kamishna wa Usalama kwa Umma Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji, pamoja na Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Rogatius
Kipali (kushoto). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba (wapili kushoto) akizungumza
na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Kamishna
Jenerali, Pius Nyambacha (kulia) wakati Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Jenerali Projest Rwegasira (katikati) alipoambatana na Naibu Katibu
Mkuu huyo katika ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, Mtaa wa
Lumumba jijini Dar es Salaam leo. Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu, Meja
Jenerali Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na
kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Kushoto ni
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Rogatius Kipali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kulia), Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba (kulia) wakiwa na
maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Kamishna
Jenerali, Pius Nyambacha (watatu kulia), wakizungumza jambo mara baada
ya Katibu Mkuu huyo kumaliza kulikagua jengo la ghorofa tano la Ofisi za
Makao Makuu ya jeshi hilo, lililopo Tazara Mchicha jijini Dar es
Salaam. Hata hivyo, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa
kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Tags
HABARI KITAIFA