BANDA MEDIA BLOG

MUIGIZAJI FILAMU IDRIS ELBA KUHUTUBIA WABUNGE UINGEREZA

Muigizaji filamu Muingereza Idris Elba anatarajiwa kuwatahadharisha wabunge kuhusiana na kukosekana kwa fursa kwa waigizaji wenye ngozi nyeusi kwenye Televisheni za Uingereza.

Muigizaji huyo ambaye naye alikumbana na hali hiyo, amesema alilazimika kwenda Marekani ili kuweza kupata kufikiriwa kupewa nafasi ya kuwa muigizaji mkuu.

Elba ameongeza kuwa watu kwenye ulimwengu wa televisheni si sawa na watu wengine waliokwenye ulimwengu halisi, hivyo televisheni zipo katika hatari ya kutoonyesha uhalisia wa jamii.

Elba mwenye miaka 43 atatoa kauli hizo wakati akitoa hotuba ya uzoefu wake Jijini London huko Westminster, na kuhudhuriwa na wabunge wapatao 100 na watendaji wakuu wa Televisheni Uingereza.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG