BANDA MEDIA BLOG

ARSENAL KAMA JANA, LEO NA KESHO

Arsenal vs Southampton
Huwezi kuitoa klabu ya Arsenal kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa msimu huu japokuwa usiku wa jana kikosi hicho kinachonolewa na Arsene Wenger kilijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Southampton wakiwa kwenye uwanja wa Emirates.
Golikipa wa Southampton Fraser Forster alikuwa shujaa wa mchezo wa jana usiku kwa kuokoa michomo ya hatari kutoka kwa wachezaji wa Arsenal.

Forster ambaye alikuwa anatoka kwenye majeruhi ya muda mrefu alikisaidia kikosi cha kocha Ronald Koeman kuondoka na pointi moja ugenini kwa kufanya saves za hatari na kuwalazimisha The Gunners kwenda sare ya bila kufungana.
Huo ulikuwa ni mchezo wa nne kwa Arsenal kwenye Premier League pasipo ushindi. Arsenal walitoka sare ya kufungana bao 3-3 na Liverpool kisha wakalazimishwa sare na Stoke City kabla ya kuchezea kibano kutoka kwa Chelsea na usiku wa jana wakashindwa tena kuchomoza na ushindi kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Southampton.
Lakini mambo yakawa machungu kwa mashabiki wa Arsenal baada ya timu zote za top six kushinda michezo yao ya jana.
Wakati zikiwa zimesalia dakika tano kabla ya mchezo kumalizika, Arsene Wenger aliwakasirisha mashabiki wa Arsenal baada ya kumuingiza kiungo mkabaji Francis Coquelin kuchukua nafasi ya Mathieu Flamini.
Arsenal wameporomoka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya England baada ya kulazimishwa sare hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG