Mchezaji Thaban Kamusoko
amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi
Disemba, 2015 baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Yanga (Amissi
Tambwe).
Kamusoko ameisaidia timu yake ya
Yanga katika michezo iliyochezwa mwezi Disemba kwa kushiriki dakika zote
katika michezo mitatu iliyochezwa mwezi wa Disemba.
Kwa kuchaguliwa kwake kuwa
mchezaji bora wa wa mwezi Disemba, Kamusoko atakabidhiwa zawadi ya fedha
taslimu shilingi milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa ligi
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Tags
MICHEZO KITAIFA