Muigizaji filamu Leonardo DiCaprio
ameshinda tuzo yake ya kwanza ya Oscar, baada ya kuteuliwa kuwania
tuzo hizo mara sita.
Akitoa hutuba yake ya kukubali tuzo
ya muigizaji bora katika filamu ya The Revenant, DiCaprio amesema
hatupaswi kuchukulia poa sayari yetu, na yeye hachukulii poa usiku wa
jana uliomtoa.
Waingereza Mark Rylance pamoja na
Sam Smith walishinda tuzo ya waigizaji bora wasaidizi na wimbo bora
wa asili. Filamu ya Mad Max: Fury Road, iliyoteuliwa kuwania tuzo 10
za Oscar, imetwaa tuzo sita.
Tags
KIBURUDANI


