Afisa
Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma
hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV)
kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez.
Vijana
nchini hususani wanaomaliza masomo ya vyuo wametakiwa kujijengea tabia
ya kufanya kazi zinazokuwepo pindi wamalizapo masomo yao na isiwe mpaka
kazi inayoanza na maslahi makubwa.
Hayo
yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma-
Ledama aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),
Alvaro Rodriguez katika warsha iliyozikutanisha taasisi mbalimbali
zinazofanya kazi kwa kujitolea za vijana.
Bi
Ledama, alisema kumekuwepo na kundi kubwa la vijana ambao wamekuwa
wakihitimu masomo yao lakini hawajishughulishi na kazi yoyote lakini
kuna wanaweza kutumia fursa zilizopo hata kwa kuanza kwa kujitolea na
kupitia kwenye kazi hiyo akajifungulia milango ya mafanikio.
Ameongeza
kuwa, Vijana wengi wamekuwa wakihitaji kazi ambazo zina maslahi makubwa
pindi tu wanapoanza kazi kwa kipindi kifupi wapate maisha mazuri bila
kutambua kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa bidii na maisha mazuri ndiyo
yanafuata.
“Ukitaka
maisha mazuri lazima ufanye kazi kwa bidii sio unataka uanze kazi
upange nyumba ya vyumba vitatu na ipo sehemu nzuri, ununue gari Mark X
na mengine mazuri lakini lazima ufanye kwanza kazi,
“Vijana
mnatakiwa kutambua kuwa ajira ni ngumu kupatikana hata kwa kuanza
kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo unaweza kuwa na juhudi na mwisho
wa siku unakuwa na maisha mazuri,” alieleza Bi Usia Nkhoma Ledama.
Afisa
Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama
akizungumza jambo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism
(KAV).
Na
kuongeza kuwa vijana wengi wasomi hawajui faida za kuanza kwa kujitolea
kuwa kunampa uzoefu na zaidi katika kuhudumia jamii kwa shughuli
mbalimbali ambazo zinakuwa na kusudi za kuelimisha jamii kuhusu mambo
mengi kwao pia kupata elimu mpya.
Kwa
upande wake, Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Walemavu, Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi.
Esther Liwa amezishauri taasisi za vijana kuwa na utaratibu wa kutoa
elimu kwenye maeneo ya wazi ili kupata nafasi ya kukutana na vijana
wengi zaidi.
Alisema
kuna kundi kubwa la vijana walio mtaani hivyo kufanya kwao maonesho ya
wazi watapata nafasi ya kutoa elimu kwa vijana walio mtaani ambapo nao
hawajapata elimu kuhusu kujiunga na taasisi hzio kwa kujitolea.
Aidha,
aliwataka vijana kutumia vitu vilivyo na asili ya Tanzania kama
utambulisho wao kama jina la warsha hiyo lilivyokuwa Kitenge – Africa –
Volunteerism (KAV).
Afisa
Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV), Stella
Karegyesa akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali (hawapo
pichani) kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake
wakati wa warsha hiyo.
Baadhi
ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge – Africa – Volunteerism
(KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni kwa
vijana, wa kwanza katika mstari wa mbele ni Mkurugenzi Msaidizi
Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa.
Warsha
hiyo iliwakutanisha zaidi ya wanafunzi 100 wa vyuo vikuu walishiriki
katika tukio hilo, wakajifunza na kuoneshwa kufurahishwa na kuhamasika
na vijana wenzao wanaofanyakazi za kujitolea ambapo iliandaliwa na
Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV) ikiwa na lengo la
kuhamasisha masuala ya kujitolea miongoni mwa vijana ambapo pia
ililihusisha shindano la vazi la kitenge na kujitolea (KAV), tukio hilo
ni kuhamasisha ili watu watambue kwamba suala la kujitolea ni sawa na
jambo la kila siku kama kuvaa vazi la kitenge.
Mmoja
wa wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV),
(kulia) akitoa maelekezo kwa mmoja wa vijana aliyohudhuria katika warsha
ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la
kuhamasisha kazi ya kujitolea miongoni kwa vijana.
Mtendaji
Mkuu wa Chama cha Vijana wa Shirika la Umoja wa Mataifa (YUNA), Arafat
Bakar akitoa maelezo kuhusu YUNA inavyofanya kazi kwa jamii ya Tanzania
na hususani vijana katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism
(KAV).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Young Tanzanian for Community Prosperty, Alfred Magehema
akitoa maelezo kuhusu taasisi yake na jinsi taasisi yake inavyofanya
kazi katika kuisaidia jamii.
Mmoja
wa Maafisa wa Raleigh Tanzania, Rose Mmbaga akitoa ufafanuzi kuhusu
taasisi yao jinsi ilivyoanza, wanavyofanya kazi na mafanikio
waliyoyapata mpaka sasa.
Meneja
wa Taasisi ya AIESEC Tanzania, Onome Ahorituwere akitoa ufafanuzi
kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi hiyo katika warsha ya Kitenge X
Africa X Volunteerism (KAV).
Pichani
juu na chini baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge
Africa Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za
kujitolea miongoni mwa vijana hao.
Washiriki wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV), wakiwa katika picha ya pamoja.
Tags
HABARI KITAIFA