Mwenyekiti wa Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) Bw. Dionis Malinzi wa pili kutoka kushoto akiongea na
wanahabari (hawapo pichani) kuhusu uteuzi wa ndugu Said Kiganja kuwa
Kaimu Katibu Mtendaji mpya wa Baraza hilo, wa kwanza kulia ni Msemaji wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Zawadi Msala na wa
kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali
watu. (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM)
………………………………………………………………………………………………………………………………………….
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo
Tanzania Deonis Malinzi amemteua Mohamed Kiganja kuwa Katibu Mtendaji
mpya wa baraza hilo baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo Bw. Henry
Lihaya kutenguliwa.
Akiongea na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti Malinzi ameeleza kuwa uteuzi huo
umekuja baada ya kuona mapungufu ya utendaji kwa aliyekuwa akishikilia
nafasi hiyo.
“Baraza la Michezo Tanzania
limefikia maamuzi haya baada ya kutoridhishwa na utendaji wa Bw. Lihaya
na hivyo Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
kufanya maamuzi ya kumtengua” alisema Bw. Malinzi
Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu
wa Sheria ya BMT namba 12 ya mwaka 1967 kifungu namba 5(1) ambacho
kinampa mamlaka Mwenyekiti wa BMT kuteua Katibu Mtendaji baada ya kupata
idhini ya Waziri mwenye dhamana.
Aidha kabla ya uteuzi huo Kiganja
alikuwani Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuanzia mwaka 2015 mpaka uteuzi wake
ulivyofanyika.
Pia aliwahi kufanya kazi kama
Afisa Mwandamizi Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania na Afisa Michezo
Mkuu katika Ofisi wa Waziri Mkuu, anashahada ya kwanza ya Elimu katika
masuala ya Michezo na Utamaduni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Tags
MICHEZO KITAIFA