………………………………………………………………………
Na.Catherine Sungura_Dodoma
Viongozi
wote kuanzia ngazi ya vijiji wametakiwa kushiriki kikamilifu katika
kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu hadi kufikia tarehe 30 machi mwaka
huu
Wito
huo umetolewa leo na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na
watoto,Ummy Mwalimu wakati alipokutana na kikosi kazi cha cha udhibiti
wa kipindupindu Mkoa wa Dodoma
“Kipindupindu
siyo suala ya afya peke yake,bali ni suala mtambuka hivyo sekta zote
zinapaswa kujumuika katika kupambana na kutokomezwa ugonjwa Huu
Ummy
alisema kipindupindu bado ni changamoto na nina janga hivyo kila mikoa
inatakiwa kuliwekea kipaumbele kwakuwa ugonjwa huo unaua kwa haraka
hivyo viongozi wote washiriki kikamilifu na si kuwaachia waganga.wakuu
wa mikoa au wilaya
Aidha
alisema licha ya kuwa na sheria ndogo Za kila halmashauri za kusimamia
usafi na mazingira lakini katika kudhibiti kuenea kwa kipindupindu
lazima liatakuja suala la kufungia biashara hususan za
mbogamboga,matunda pamoja na chakula”suala la kukusanya mapato lipo na
litaendelea kuwepo lakini suala la kipindupindu linapoteza maisha,maisha
hayatafutwi lakini pesa zinatafutwa lakini ukikosea utapoteza maisha ya
watu wengi”
Ummy
alisema tangu kipindupindu kiingie nchini agosti mwaka jana,halmashauri
zimetumia pesa nyingi katika kutokomeza ugonjwa huo,lakini wangeweza
kuzuia mapema,pesa hizo.zingeenda kutatua tatizo la madawati katika
shule za msingi nchini
“Mnapoona
hamjaridhika na uendeshaji wa migahawa,msisite kuzifungia mara
moja,mapato mtakusanya haraka kwa kuwa na nguvu za pamoja baada ya
kutokomeza ugonjwa na kuweza kuingiza mapato mengi na kwa haraka tofauti
na kuwa na hilo tatizo
Hatahivyo alizitaka vikosi vyote vya mikoa nchi,kuwashirikisha wadau wote wakiwemo viongozi wa dini zote kuweza kuelimisha kuweza kutoa elimu ya jinsi gani ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kwa waumini wao
Hatahivyo alizitaka vikosi vyote vya mikoa nchi,kuwashirikisha wadau wote wakiwemo viongozi wa dini zote kuweza kuelimisha kuweza kutoa elimu ya jinsi gani ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kwa waumini wao
Mkoa
wa dodoma umetumia takribani shilingi milioni 124 za kitanzania toka
kipindupindu,hadi leo kuna wagonjwa wanne katika kambi ya kipindupindu
wilaya ya bahi,jumla ya wagonjwa 450 waliugua na vifo12,wilaya
zilizoathirika ni bahi,dodoma mjini na chamwino
Tags
AFYA