Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imesema
kuwa makampuni binafsi ya ulinzi yanayofanya kazi bandarini hayahusiki
na ulinzi wa sehemu nyeti za Mamlaka hiyo.
Akitoa ufanuzi huo leo jijini Dar es salaam,
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Janeth Ruzangi amekiri kuwepo
kwa makamuni yanayofanya kazi ya ulinzi bandarini akifafanua kuwa
hayahusiki kwa namna yoyote ile kulinda sehemu za ndani za ofisi
zilizoko bandarini.
“Ninapenda kuwafahamisha wananchi kuwa
Bandari inalindwa na walinzi wa aina tatu ; Jeshi la polisi, Polisi
wasaidizi walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (Auxilliary
Police) pamoja na walinzi wa Makampuni binafsi”
Ameongeza kuwa makampuni binafsi ya ulinzi
hayalindi sehemu nyeti za bandari bali yanalinda nje ya bandari kama
ilivyo kwenye ofisi zingine.
Ameongeza kuwa,polisi walioajiriwa na
Mamlaka ya Bandari Tanzania wako kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na
Bunge na wamepata baadhi ya mafunzo ya kipolisi.
Ikumbukwe kuwa agizo la kuwandoa walinzi wa
makampuni binafsi kwenye maeneo nyeti ya bandari lilitolewa na Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mwezi Februari mwaka huu.
Tags
HABARI KITAIFA