| Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana akiteta jambo na Balozi wa China Dkt, LU Youqing. |
MKUU wa
Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mwishoni
mwa wiki amekutana na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing na
kuzungumzia masuala ya kukuza uwekezaji na ushirikiano baina ya pande hizo
mbili.
Rugimbana
amemwelezea Balozi huyo ofisini kwake mjini Dodoma kuwa ameunda kikosi kazi cha
Masuala ya Uwekezaji ambacho kina kazi ya kuboresha mazingira ya uwekezaji,
kutambua wawekezaji waliopo na changamoto zinazowakabili na njia bora za
kuzitatua kwa lengo la kuboresha mazingira na kukuza uwekezaji Mkoani humo.
Amesema
kwa sasa anataka kuanzisha eneo maalum la uwekezaji kwenye Mkoa wa Dodoma
ambapo kitaundwa kituo chenye kutoa huduma zote zinazohitajika kwenye uwekezaji
na kutakuwa na taasisi zote zinazohusika na utoaji wa huduma hizo ambapo
mwekezaji akifika kituoni hapo hana haja ya kuondoka kwenda kutafuta huduma
sehemu nyingine, mahitaji yake yote yatatatuliwa hapohapo kituoni na mara moja
ataanza shughuli yake ya uwekezaji.
| Balozi wa China Nchini Dkt, Lu Youqing akiwa na ujumbe wake walipotembelea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma |
| RUGIMBANA NA DKT, LU |
Vilevile,
Balozi wa China alimhakikishia Rugimbana kuwa
atasaidia kuzikutanisha Mamlaka zinazoshughulikia ujenzi wa mji mpya wa
serikali na serikali kuhamia Dodoma na mamlaka ya Manispaa ya Jiji la Beijing
China ambayo inauzoefu na imefanikiwa kujenga mji mpya mbali na ule wa zamani
kwa kipindi cha miaka miwili tu, lengo likiwa kubadilishana uzoefu katika
kutekeleza mradi huo wenye manufaa makubwa kiuchumi hapa Tanzania.
Tags
HABARI KITAIFA