BANDA MEDIA BLOG

Mkutano Mkuu Wa Mwaka wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya wafanyika Mkoa wa Shinyanga


Hapa ni katika Msikiti wa Masjid Latif Ahmadiyya Muslim Jamaat Nsalala uliopo kijiji cha Nsalala ,kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga ambapo leo Jumapili Mei 22,2016 Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga(Ahmadiyya Muslim Jamaat Shinyanga) imefanya mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Shinyanga ukiwa na kauli mbiu ya ” Love For All Hatred For None (Mapenzi Kwa Wote Bila Chuki Kwa Yeyote”.
….
Mgeni rasmi alikuwa katibu tawala msaidizi idara ya  uchumi na uzalishaji aliyemwakilisha kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga John Mongella huku waumini wa dini hiyo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wakihudhuria mkutano huo.
Mkutano huo uliolenga kuhamasisha amani katika jamii kwa kuwakumbusha waumini kumjua mwenyezi mungu hali itakayosaidia kupunguza hata kumaliza kabisa vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya watu wasio na hatia kama vile vikongwe na albino, umehudhuriwa pia na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry (pichani juu).
Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry alieleza kusikitishwa na kitendo cha mauaji ya watu watu msikitini na kuongeza kuwa dini ya kiislam hairuhusu vitendo kama hivyo huku akiviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi ili kubaini wahusika wa kitendo hicho haramu.
Kupitia mkutano huo jamii imeelimishwa juu ya dhana potofu dhidi ya uislamu ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha dini hiyo pamoja na vikundi vya kigaidi mfano wa Boko haram, Isis, Al-shabaab na vingine vingi ambavyo vimekuwa vikidhuru binadamu. 
Mada mbalimbali zimetolewa na viongozi wa jumuiya hiyo ikiwemo nafasi ya dini katika maisha ya binadamu,malezi ya watoto na majukumu ya wazazi sawa na mafundisho ya dini ya kiislamu,umuhimu wa kuwa kiongozi (Khalifa) wa kiroho na barakaza ukhalifa pamoja na masharti ya kujiunga na jumuiya hiyo(masharti 10 ya Baiat na wajibu wa waumini.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa mkutano huo,ametusogezea picha 55 kilichojiri..
Hapa ndipo Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga waumini wa dini ya kiislamu kutoka Jumuiya hiyo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wamejitokeza kwa wingi kusikiliza mawaidha mbalimbali kutoka kwa viongozi wa Jumuiya hiyo pamoja na wageni waalikwa akiwemo kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mohammed Idd Nchira
Bango likionesha kilichokuwa kinaendelea 
Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya nchini Tanzania Abdulrahman Mohammed Ame akitoa mada kuhusu Haja ya nafasi ya dini katika maisha ya binadamu ambapo alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kutenda mambo mema na kujiepusha na vitendo vya kihalifu ikiwemo kuua watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.
 
Alisisitiza kuwa uislamu ni dini ya amani hivyo kuwataka binadamu kuishi kwa amani na kwamba kitendo cha kuua mtu mmoja ni sawa na kuua dunia nzima.Hata Hivyo Ame alisema sera ya jumuiya hiyo ni kutochanganya siasa na dini .
Meza kuu,wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry,kushoto kwake ni mgeni rasmi Mohammed Idd Nchira,akifuatiwa na rais wa Jumuiya hiyo Kanda ya Ziwa Salim Thani,wa kwanza kushoto ni Naibu rais wa jumuiya hiyo Kanda ya ziwa Yahaya Kamba Ulaya.Wa kwanza kulia ni Mbashiri wa kanda ya ziwa  wa jumuiya hiyo Sheikh Waseem Khan 
Waumini wa dini ya Kiislam kutoka maeneo ya mjini na Vijijini ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga waliojitokeza katika mkutano huo
Mgeni rasmi katika mkutano huo Mohammed Idd Nchira akiwahutubia waumini wa dini ya kiislamu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG