Na Tiganya Vincent_MAELEZO-Dodoma.
Serikali kwa kushirikiana na
wadau wa ndani na nje ya Nchi wameifanyia maboresho Sera ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2003 na kuja ya sera mpya ya mwaka
2016 ili kuunganisha sekta muhimu za uzalishaji na viwanda katika
miundombinu ya TEHAMA.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia
Edwin Ngonyani wakati wa uzinduzi wa Sera ya Tekonolojia ya Habari na
Mawasiliano ya mwaka 2016.
Alisema kuwa hatua hiyo
inalenga kuiwezesha Tanzania kutumia fursa zinatokana na uwepo wa
miundombinu ya TEHAMA kuingia katika uchumi wa kati ifakapo 2025 kwa
kuimarisha matumizi ya TEHAMa katika sekta mbalimbali za uzalishaji
nchini.
Mhe. Ngonyani aliongeza kuwa
Sera hiyo ni muhimu katika kujenga jamii habari itakayowezesha nchi
kufikia maarifa yatakayosaidia kwenda sanajari na mpango wa Taifa
kujenga uchumi wa viwanda.
Alisema kuwa Sera hiyo
imejikita katika kukuza matumzi TEHAMA katika uzalishaji ili kuongeza
tija , kukuza utafiti na kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi katika
TEHAMA kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Awali akiongea kabla ya
uzinduzi wa Sera hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano(Mawasiliano) Profesa Faustin Kamuzora alisema kuwa Sera
hiyo itasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji wa kazi wa kila siku katika
sekta mbalimbali nchini.
Alisema kuwa sera hii itasiaidia kwenda sanajari ya ukuaji wa kasi wa matumzi ya mawasiliano hapa nchini.
Tags
HABARI KITAIFA